Je ni kweli ada ya mtihani wa kidato cha nne ni tshs 50,000/=

Je ni kweli ada ya mtihani wa kidato cha nne ni tshs 50,000/=

SOSDANNY

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
453
Reaction score
444
Za mchana wakuu.
Nilipigiwa simu na ndugu yangu alioko mbali na ninapoishi. Akaniambia kuwa anahitaji nimsaidie ada ya mtihani wa form four,nikamuliza ni shilingi ngapi? akaniambia Tshs 50,000/= Nikashangaa!! Nikajua anataka kunipiga changa la macho. Wananchi hebu mnifahamishe ni kweli? Kama ni kweli nyinyi wananchi mnasemaje? Binafsi kama ni kweli naona hayo maisha bora kwa kila mtannzania hayapo. Kwa walioko mjini hebu tujadili hili.
 
Kama ni wa QT inawezekana
.
Ila hawa wa kawaida inaanzia
35,000 kwa kadiri unavyo chelewa inapanda kila baada ya mwezi...
.
Kiasi cha kama 15000 hivi kila mwezi if am not mistaken
.
Lipa mapema kuepuka usumbufu
Tunakutakia Siku Njema BB: NECTA
.
Tumetoa Tangazo Hili kwa CSEE 2014 soma hapa
.
Toa Taarifa ya cheti Kilichopotea hapa
vyeti@necta.go.tz
.
AHSANTE
 
Wananchi hebu mnifahamishe ni kweli? Kama ni kweli nyinyi wananchi mnasemaje?

Kwanza wewe ambaye sio mwananchi (kwa maana ya kwamba ni kiongozi) ulilichukuliaje mheshimiwa sana?
 
Kwa nilivyomuelewa labda kakuomba both ya mock na necta maana mock ni sh 15,000 na necta 35,000 jumla 50,000 hata sisi tuliambiwa tutoe pia hiyo ili tulipie zote.

Pia yaweza kuwa hiyo 15,000 yaweza kuwa ni penalti ya kuchelewa kulipa ingawa sina uhakika ila nakumbuka feb ndio mwisho wa kulipia 35,000 ukizidisha march unalipa na penalti. Ila hada kamili ya kulipia necta ni 35,000/-
 
kama ni adhabu ni sawa kwa maaana kama amechelewa kulipia kwa muda uliopangwa ila bei yake halali bila penati ni 35,000/ na kama ni pc yaani mtahiniwa wa kujitegemea kuna pesa ya kituo cha kufanyia mtihani ambacho atalipia kuanzia sh 10,000/= mpaka 30,000/=
 
mkuu kwa waraka na barua wanatakiwa kulipa 50,000/- tena kwa kipindi fulani baada ya hapo kuna penalt kama unataka maelezo ni pm namba yako nikupe
 
mkuu kwa waraka na barua wanatakiwa kulipa 50,000/- tena kwa kipindi fulani baada ya hapo kuna penalt kama unataka maelezo ni pm namba yako nikupe
Sawa nimeelewa kwani aliniambia ada ya mtihani wa NECTA ni Tshs 50,000/= bila penalt na MOCK EXAMS ni Tshs 15,000/= jumla ni Tshs 75,000/=. Naona sasa hata elimu imekuwa anasa, poa tutakwenda hivi hivi mdogo mdogo. Nashukuru kwa maelezo yenu.
 
Ni tzs 50,000 kwa private & QT seaters.

Ila not sure kwa QT seater,if not it might be tzs 35,000.

Kindly Visit: www.necta.go.tz
 
Kwa Private & QTs,apo bado fee ya kituo hujajumlisha na mwisho tar 28/02 bada ya apo kuna penalty ya exam fee na mwaka jana ilikuwa 25,000/=
 
Za mchana wakuu.
Nilipigiwa simu na ndugu yangu alioko mbali na ninapoishi. Akaniambia kuwa anahitaji nimsaidie ada ya mtihani wa form four,nikamuliza ni shilingi ngapi? akaniambia Tshs 50,000/= Nikashangaa!! Nikajua anataka kunipiga changa la macho. Wananchi hebu mnifahamishe ni kweli? Kama ni kweli nyinyi wananchi mnasemaje? Binafsi kama ni kweli naona hayo maisha bora kwa kila mtannzania hayapo. Kwa walioko mjini hebu tujadili hili.

Mwombaji ni mkweli kabs na inaonekan wana JF wengi hauna ufahamu wa hilo kwa mujb wa waraka wa baraz la mithan ada ya mthan wa kidato cha nne ni 50,000 na mwsho bila penalt ni 28 feb na baad ya hapo 65,000 na akibachlw had laki!
 
tuache utani, elimu yetu itaendelea kushuka kila mwaka. Kama ada ya mtihani wanapandisha kama pledge za harusi bila kutoa pubic notes sidhan kama kuna tupo serious na elim yetu. Au ndo imepanda sambamba na umeme na maji? Nawashauri wanafunzi wawakomoe NECTA kwa kufaulu kwa wingi tuone kama wataendelea kupandsha.
 
ADA ya Mtihani ni 50,000/=. na tarehe ya mwisho ni tar 28 inapanda kuwa 65,000/= hii ni kwa mujibu wa barua zilizotumwa mashuleni toka NECTA
 
tuache utani, elimu yetu itaendelea kushuka kila mwaka. Kama ada ya mtihani wanapandisha kama pledge za harusi bila kutoa pubic notes sidhan kama kuna tupo serious na elim yetu. Au ndo imepanda sambamba na umeme na maji? Nawashauri wanafunzi wawakomoe NECTA kwa kufaulu kwa wingi tuone kama wataendelea kupandsha.

taaarifa imetolewa kwa barua zilizotumwa mashuleni toka NECTA
 
Mkuu dogo, kaniambia hivyo hivyo nikajua ameanza utapeli na hivyo nikalazimika kufanya uchunguzi kumbe kweli ni 50000/=
 
tuache utani, elimu yetu itaendelea kushuka kila mwaka. Kama ada ya mtihani wanapandisha kama pledge za harusi bila kutoa pubic notes sidhan kama kuna tupo serious na elim yetu. Au ndo imepanda sambamba na umeme na maji? Nawashauri wanafunzi wawakomoe NECTA kwa kufaulu kwa wingi tuone kama wataendelea kupandsha.
Unajua kilichonishangaza sikusikia hata tangazo redioni kuhusu huu upandaji wa ada ya NECTA, halafu ada ya shule kwa mwaka ni tshs 40,000/- na unalipa kidogo kidogo, lakini huku vijijini wazazi wanashindwa kulipa hiyo ada, sasa hii ya 50,000/= kwa mkupuo itakuwaje? na kwa muda mfupi hivi? Mimi nafikiri wanatakakuzuia matokeo ya wadogo zetu. NECTA ilitazame vizuri binafsi sioni kama ni sawa.
 
Back
Top Bottom