SI KWELI Je ni kweli Bangi Ekari 10 zimepatikana Kwenye shamba La Askofu Mwamakula

SI KWELI Je ni kweli Bangi Ekari 10 zimepatikana Kwenye shamba La Askofu Mwamakula

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo Na Taarifa Ambayo Imechapishwa Kwenda mtandao wa Facebook Ikieleza kuwa Bangi Ekari 10 zimepatikana Katika Shamba la Askofu Emmaüs Bandikile..je Taarifa Hiyo Ina Ukweli Kiasi Gani.

ekari.jpg
 
Tunachokijua
Askofu Emmaus Mwamakula ni Askofu mkuu wa makanisa ya Moravian Uamsho Tanzania. Mwamakula amekuwa pia akijotoeza hadharani na kukosoa changamoto zozote zinazojitokeza ama kufanywa na serikali.

Madai

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Facebook amechapisha taarifa yenye utambulisho wa Jambo TV ukiw ana ujumbe unaosomeka kuwa;

Bangi ekari 10 yakamatwa Shambani kwa Askofu Emmaus Bandikile Mwamakula Mlima RUngwe, Mbeya

Uhalisa wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa madai hayo si ya kweli.

Kupitia ufuatiliaji wake kwa kuzingatia vyanzo vya kuaminika, imebainika kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminka kilichotoa taarifa hiyo ukilinganisha na uzito wake.

Aidha hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na Jeshi la Polisi ama mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) kuhusu jambo hilo.

Askofu Mwamakula kupitia ukurasa wake wa Facebook ambao amekuwa akiutumia mara kwa mara amechapisha taarifa kuonesha kudhihaki madai hayo, Askofu aliandika kuwa;

Lile shamba la ekari 10 za bangi mlilomgea askofu kule Mlima Rungwe Kauzeni ili wapwa zenu wapate pesa za kuendeshea serikali maaana EU wanakata misaada

Hata hivyo grafiki iliyotumika pia ni ya kughushi na haikuchapishwa na Jambo TV, aidha aina ya mwandiko uliotumika hautumiwi na chanzo hicho.
Back
Top Bottom