Je, ni kweli bei ya mafuta Zanzibar iko chini kuliko huku Bara?

Je, ni kweli bei ya mafuta Zanzibar iko chini kuliko huku Bara?

sitagliptin

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2023
Posts
1,501
Reaction score
2,935
Naomba kujua sio kwa ubaya pia kwanini Tanzania bara na Zanzibar bei ya mafuta zinapishana sana?
Bei ya Tanzania 4000 lakini Zanzibar ni 2900.

Sisi ni nchi moja ila kwann tunatofaut kubwa sana hapa.

Kwanini mamlaka zetu wajifunze kwa wenzetu?
 
Zanzibar mpaka leo kuna sehem naul yake ni 500. Bara nauli ya 500 ipo?
 
Zanzibar tuna mamlaka yetu inaitwa ZURA so wao tarehe 8 ya kila mwezi ndo hutangaza bei mpya ya mafuta kwaio msituonee choyo jamani na sisi zamu yetu itafika tuu
 
Ndo faida ya kutoa marais wawili sehemu moja hiyo
Nadhani hili lisitokee tena Tanzania, kama zanzibar wanataka nawao kuongoza Tanzania basi waondoe utaratibu wa kuwa na rais wa zanzibar. Haiwezekani nchi ikawa na marais 2 halafu wote wanatoka upande mmoja wa muungano.
 
Naomba kujua sio kwa ubaya pia kwanini Tanzania bara na Zanzibar bei ya mafuta zinapishana sana?
Bei ya Tanzania 4000 lakini Zanzibar ni 2900

Sisi ni nchi moja ila kwann tunatofaut kubwa sana hapa,

Kwann mamlaka zetu wajifunze kwa wenzetu?

Ni kweli hadi leo bei ni 2,900.

Na Kwa Zanzibar, ZURA inatangaza bei za mafuta tarehe 7 ya kila mwezi na bei husika (endapo ina mabadiliko) inaanza kutekelezwa tarehe 8 au 9. Ndio utaratibu uliopo hata pale ambapo hakuna mabadiliko ya bei tarehe 7 lazima itatoa taarifa kuhusu bei ya mafuta.

Kwahiyo tutegemee yatapanda pia.
 
Nadhani hili lisitokee tena Tanzania, kama zanzibar wanataka nawao kuongoza Tanzania basi waondoe utaratibu wa kuwa na rais wa zanzibar. Haiwezekani nchi ikawa na marais 2 halafu wote wanatoka upande mmoja wa muungano.

Kwani Mwinyi ni Mzanzibari ?
Mkuu mambo ya CCM kuyaelewa ni ngumu sana, Kila siku raisi wa Zanzibar anachaguliwa Chamwino unafikiri Zanzibar wanafurahi?
 
Back
Top Bottom