Je, ni kweli chokaa inachangia ubora na ufanisi wa mbolea katika kilimo cha ndizi?

Je, ni kweli chokaa inachangia ubora na ufanisi wa mbolea katika kilimo cha ndizi?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Nilikiwa kwenye Mkoa wa Kagera ambapo kuna mwenendo unaoongezeka wa wakulima wa ndizi kutumia chokaa katika mashamba yao. Wakulima hao wanadai kuwa matumizi ya chokaa husaidia migomba kustawi vizuri na kupunguza au kuzuia mashambulizi ya baadhi ya wadudu wanaosababisha kudhoofika au kuharibika kwa migomba.

Aidha, inaelezwa kuwa chokaa inapochanganywa na mbolea ya kawaida huongeza ubora na ufanisi wa mbolea hiyo, hivyo kuchangia uzalishaji bora wa ndizi.
photo_2026-01-07_14-14-32.jpg

Kutokana na kasi ya jambo hili linaloendelea kusambaa miongoni mwa wakulima, ningependa kufahamu kama matumizi ya chokaa katika kilimo cha ndizi yamefanyiwa utafiti wa kisayansi. Je, ni kweli chokaa ina uwezo wa kutatua changamoto za wadudu na kuboresha ustawi wa migomba kama inavyodaiwa?

Naomba wataalamu wa kilimo au taasisi husika watusaidie kutoa ufafanuzi sahihi juu ya suala hili, ili wakulima wapate mwongozo unaotegemea ushahidi wa kitaalamu.

Inabidi upime PH kwanza ya udongo maana ndizi pH yake iwe 5.5-7.

Angalia aina ya udongo usije kuwa alkaline kali.

chokaa uwongeza acid ya kama itakuta hipo.

kazi yake kubwa kurekebisha tindikali ya udongo.
 
Kwenye ufugaji wa Mbuzi chokaa tunaimwaga chini kwenye mabanda kwaajili ya kuwafukuza viroboto huwa weupe wake unawafanya wanashindwa kujificha kwenye vumbi na sehemu za ukutani na kwenye nyufa maana kiroboto ni mweusi na husumbua sana ustawi wa mifugo.
 
Sizani kama kuna ukweli wowote ninalima migomba kwa mda mrefu sana nachoweza kusema ni kupata mbegu bora iwe ya kiasili au kisasa , chimba mashimo yaache kwa miezi mitatu ndo uchanganye mbolea na kupanda , sehemu kame umwagilie na ujitahidi kuwa na mbolea ya kutosha sana , pia migomba inapoelekea kuchanua unaweza ongeza mbolea ya MOP inafanya vizuri zaidi .
Kuhusu chokaa ni nzuri kupunguza asidi lakini nina uzoefu niliweza kuanzisha shamba la ndizi eneo lililokuwa shamba la chai na zilifanya vizuri( unaweza kugoogle chai inastawi katika tindikali ya ngapi) nilitumia mbinu mbili ya kuweka mbolea nyingi na kumwaga pumba za mchele kisha kukatua hilo shamba hadi sasa maendeleo ni mazuri sana
 
Wapi huko mkuu?!
 
Kwenye fugaji wa Mbuzi chokaa tunaimwaga chini kwenye mabanda kwaajili ya kuwafukuza viroboto huwa weupe wake unawafanya wanashindwa kujificha kwenye vumbi na sehemu za ukutani na kwenye nyufa maana kiroboto ni mweusi na husumbua sana ustawi wa mifugo.
shukrani.
 
Back
Top Bottom