Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Wana jamvi, leo tulikuwa na ubishi juu ya maambukizi ya ukimwi, jambo tuliloshindwa kufikia muafaka ni kuhusu damu inayotoka siku ya hedhi, naomba nililete kwenu ki hivi; inasemekana kuna uwezekano wa mama mwenye VVU Kujifungua mtoto aliyesalama, na ni kweli kuwa mtoto ni matokeo ya yai lililorutubishwa na mbegu za kiume ambapo yai hilo lisiporutubishwa hutoka kama damu siku ya hedhi! sasa je, endapo mwanamke ameadhirika yai linalotoka kama damu siku ya hedhi,damu ile ina VVU au la!? nawasilisha!