Je ni kweli dna ikipimwa na mzazi mmoja majibu sio sahihi asilimia 100?

Je ni kweli dna ikipimwa na mzazi mmoja majibu sio sahihi asilimia 100?

sumbwasumbwa

Member
Joined
Oct 4, 2013
Posts
32
Reaction score
6
Nimeshangaa pale nilipopewa majibu ya DNA niliyokwenda kumpima mtoto wangu pamoja na mimi pale Ocean Road na ikaandikwa katika karatasi ya matokeo kwamba sio asilimia 100 sahihi kwasababu vipimo havijamuusisha mama yake.

Hivi majuzi nilimchukua mtoto wangu nikaamua kwenda kumpima DNA ili kuhakikisha kama sijabambikiwa, lakini katika hatua zote hizo sikumshirikisha mama yake wala kumjulisha kwa njia moja au nyingine.

Chakushangaza, majibu yalivyotoka (yalikuwa positive) ila yakasema majibu sio sahihi kwa asilimia mia kwasababu hayakumhusisha mmoja wa wazazi yaani mama mtu,,,kitendo kile sikukielewa na nilivyouliza walisema inavyotakiwa ni lazima mpime mama, baba na mtoto / watoto husika ili kipimo kiwe sahihi asilimia mia.

Duh nikashangaa kiasi fulani.
 
Back
Top Bottom