Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Nimepata kutazama mahojiano ya Sylvester Stallone na mtandao wa Vulture na kuona akidai kuwa walipokuwa wakirekodi filamu ya Rocky IV, toleo la nne basi alikutana na majanga nusu kupoteza maisha kwani Dolph Lundgren alimpiga ngumi walipokuwa wakirekodi vipande vya mapigano. Alidai kuwa alitamani kutengeneza filamu bora hivyo alimpa maelekezo Dolph Lundgren kupiga ngumi za ukweli, na hizo ngumi nzito kiasi ndo zilipekea hali ya kiafya ya Sylvester Stallone kuwa mbaya na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Je taarifa au mahojiano haya yana ukweli ndani yake au ndo promo za wasanii?