#COVID19 Je, ni kweli hakuna Corona Tanzania?

#COVID19 Je, ni kweli hakuna Corona Tanzania?

Tanzania nasikia kuna tatizo la upumuaji, mana sio kila kifo kinatokana na UVIKO
 
unallazimisha nchi yetu iwe na korona ili unufaike na nini haswa?

"mchawi" tu ndiye humuombea matatizo mwenzake hiyo ndio furaha yake kuona binaadamu anateseka na hata kufa.
jamani tuache roho za kichawi.

kama tulivyo elekezwa tuendelee kuchukua tahadhari, tutumie dawa zetu za asili huku tukizidi kumuomba Mungu atuepushe na janga hili na hakika Tanzania itaendelea kuwa nchi salama kwa uwezo wake Mungu.
 
Za kuambiwa changanya na zako.Tanzania hamna Corona chukua hatua.Leo Mwamposa alikuwa mkali Sana anataka watu wakae mita 1.Na imemlazimu kufanya ibada 5 ili kuwafikia watu wote bila msongamano.Nashangaa hapa KKT kijitonyama watu hata hawajali Rev Dk Eliona Kimaro chukua tahadhali Sana.mjini Kuna vumbi gari zinazima.Sio kila kifo ni Corona ila ukiondoka kipindi hiki utaacha stori za Nimonia.
 
Kama Uingereza, Zanzibar, Madagascar, nk nchi ambazo ni visiwa zina hayo maambukizi ya Corona! Iweje Tanganyika iliyozungukwa na nchi nyingine karibia pande zote, ikose?

Akili za mbayuwayu, changanya na zako. Tuendelee kuchukua tahadhari. Tusikubali kuamuliwa hatma ya maisha yetu na mtu mmoja tu, na ambaye kwa upande wake akiwa anapata ulinzi wa maisha yake kwa % zaidi ya 1000!
 
Back
Top Bottom