- Source #1
- View Source #1
Wakuu, naomba tu kuuliza. Njia ya kifo cha mende wakati wa tendo ndio njia rahisi ya mwanamke kupata ujauzito kwa haraka? Au ikoje ikoje hii?
- Tunachokijua
- Ujauzito ni kipindi ambacho kijusi kimoja au zaidi hukua ndani ya kizazi. Mara nyingi ujauzito hutokea baada ya kufanya tendo la ndoa, lakini unaweza pia kutokea kupitia njia za kiteknolojia za kusaidia uzazi.
Mayai ya uzazi huhifadhiwa kwenye ovari. Katika kila mzunguko wa hedhi, ovari hutoa yai moja. Yai hilo husafiri taratibu kupitia mrija wa uzazi (fallopian tube), ambako husubiri mbegu ya kiume. Mchakato huu, unaoitwa upevushaji (ovulation), huchukua takribani saa 12 hadi 24.
Madai
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na madai kuwa kuna baadhi ya mitindo ya kufanya tendo la ndoa inaweza kusaidia mtu kupata ujauzito hata kama amekosa uajauzito kwa muda mrefu. Huku madai mengine yakieleza kuwa aina ya mtoto inaweza kuchangia kuchagua jinsia ya mtoto atakayezaliwa.
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia machapisho na tafiti za kisayansi n akubaini kuwa madai hayo yanapotosha uhalisia na yanasalia kuwa nadharia tu kwani hayana msingi wa kisayansi.
Tovuti ya WebMed inabainisha kuwa hakuna mkao wowote wa kufanya tendo la ndoa ambao umethibitishwa kuongeza uwezekano wa kupata mimba. Kinachoweza kusaidia ni kuweka shahawa karibu na mlango wa kizazi (cervix), ambao ni njia inayounganisha uke na mfuko wa uzazi.
Hakuna tafiti zilizochapishwa wala ushahidi wa kisayansi wenye hitimisho la wazi unaoonyesha kuwa mkao wa kufanya tendo la ndoa una mchango mkubwa katika kuongeza uwezekano wa kupata mimba.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanapendekeza mikao inayoruhusu uume kuingia ndani zaidi inaweza kuongeza nafasi ya kutungwa kwa mimba. Nadharia hii inatokana na dhana kwamba kuingia kwa kina zaidi kunaweza kufanya shahawa zimwagwe karibu zaidi na mlango wa kizazi (cervix).