POTOSHI Je, ni kweli hii sauti inatolewa na kichwa cha treni ya SGR?

POTOSHI Je, ni kweli hii sauti inatolewa na kichwa cha treni ya SGR?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha


Screenshot 2026-04-20 112009.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikionesha kichwa cha treni ya SGR kikiwa kinatoa sauti yenye muungurumo usio wa kawaida.


Je, ni upi uhalisia?

Sauti inayosikika kwenye video si ya injini ya treni ya umeme. Ni sauti ya gari.

Kutofautiana kwa "Pitch" na Mwendo, sauti inaonesha mabadiliko ya gia na muungurumo wa juu ambao hauendani na mwendo thabiti wa treni ya umeme.

Treni za mwendokasi (SGR) zinazotumia mfumo wa umeme (Electric Multiple Unit - EMU) hazitumii injini za mwako wa ndani (Internal Combustion Engines). Kwa asili, treni hizi zina sauti ndogo sana (humming sound) inayotokana na msuguano wa magurudumu kwenye reli na upepo, si mngurumo wa mlipuko wa moshi kama unavyosikika.

Kutokana na kipande hicho cha video Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa Taarifa kwa umma kuuarifu kuhusu video hiyo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba siyo ya kweli ni uzushi.

Taarifa hiyo inabainisha kuwa baada ya kufuatilia kwa makini, Shirika linathibitisha kuwa treni zote za SGR zinafanya kazi kwa ufanisi na ziko katika hali salama kabisa, aidha hakuna tukio lolote lililoripotiwa linalohusiana na hitilafu ya aina hiyo kama inavyoonekana kwenye video hiyo.

TRC imeongeza kuwa usalama wa abiria na mali zao ni kipaumbele cha juu, na mifumo yote ya kiuendeshaji wa treni hukaguliwa mara kwa mara na wataalamu ili kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa kwa ubora na usalama wa hali ya juu huku shirika hilo likiwaomba wananchi kupuuza na kutoendelea kusambaza taarifa hizo zisizo sahihi, na badala yake kupata taarifa sahihi kupitia vyanzo rasm.​
Back
Top Bottom