SI KWELI Je, ni kweli John Heche Julai 7 alitoroka kupitia mpaka wa Sirari na kuelekea Nairobi hadi Ubelgiji?

SI KWELI Je, ni kweli John Heche Julai 7 alitoroka kupitia mpaka wa Sirari na kuelekea Nairobi hadi Ubelgiji?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
1783488544579.png

1783488518055.png
 
Tunachokijua
Madai

Yericko Nyerere amabaye ni mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), ambaye pia amekuwa akijitambulisha kama mwandishi wa vitabu kupitia ukurasa wake wa Facebook amechapisha picha ya tiketi ya kielektroniki inayoonesha abiria anayeitwa John Wegesa Heche ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisafiri kutoka Nairobi (NBO) kwenda Brussels (BRU) kupitia Amsterdam (AMS) tarehe 07 Julai 2026, huku akidai Heche kupanga Maandamano ya Julai 07, na yeye akitoroka kwenda nje ya nchi.

Je, ni upi uhalisia?


Baada ya kufanya uchunguzi wa kidijitali na uhakiki wa vipengele vya kiufundi vilivyomo kwenye picha ya tiketi hiyo, JamiiCheck imebaini kuwa nyaraka hiyo ni ya kughushi kwa sababu zifuatazo:

1. Namba ya Tiketi (E-Ticket) Haiendani na Shirika la Ndege: Kila shirika la ndege duniani lina namba maalum ya utambulisho wa tarakimu tatu (Airline Prefix) inayomilikiwa na Umoja wa Kimataifa wa Usafiri wa Anga (IATA).

Tiketi hii inaonyesha namba 1765060835803.

Namba ya mwanzo 176 ni utambulisho maalum wa shirika la ndege la Emirates.

Hata hivyo, tiketi hiyo inadaiwa kuwa ni ya KLM Royal Dutch Airlines, ambayo namba yake ya utambulisho rasmi ni 074. Haiwezekani mifumo ya kiotomatiki itoe tiketi ya KLM inayofunguliwa na namba ya Emirates.

2. Maelezo ya Mawasiliano ya Wakala ni ya Kufikirika (Placeholders): Katika ukurasa wa pili, kwenye kisanduku cha wakala aliyetoa tiketi hiyo (Issued By: EMD TRAVEL COMPANY LIMIT), anwani na namba za simu zilizowekwa ni zile zinazotumiwa kwenye mifano ya fomu (templates) na sio mawasiliano halisi ya kibiashara:

Sanduku la Posta: P.O. Box 12345 (Hii ni namba ya mfano inayotumiwa duniani kote kwenye fomu za majaribio).

Namba ya Simu: +254 20 1234567 (Mfuatano wa namba 1 hadi 7, unaonyesha wazi kuwa ni namba ya kufikirika).

3. Makosa ya Kiufundi katika Mpangilio wa Safari (Layout & Itinerary)
Mifumo ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Tiketi (GDS) kama Amadeus au Sabre haizalishi makosa ya mpangilio (formatting errors) yanayoonekana kwenye nyaraka hii:

Mchanganuo Unaojipinga: Kichwa cha habari cha safari ya kwanza kinataja kuwa safari ni kutoka Nairobi kwenda Brussels kupitia Amsterdam. Hata hivyo, jedwali la mchanganuo wa chini yake limeacha kabisa kipande cha pili cha safari (Amsterdam kwenda Brussels) na kuonyesha kipande cha kwanza tu.

Nyaraka inayosambazwa sio tiketi halisi ya kusafiria bali ni fomu iliyotengenezwa kwa kutumia programu za kompyuta (graphic editing/template) kwa kutumia taarifa za uongo.


Taarifa kutoka kwa uongozi wa CHADEMA

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) John Mnyika amekanusha taarifa hiyo na kwamba si ya kweli. Akikanusha madai hayo Mnyika amesema:

"Nimempata Heche, hiyo ni taarifa potofu, yupo nchini anaendelea na shughuli zake kama kawaida na baadaye tutatoa picha kupitia mitandao yetu akiwa kwenye shughuli za kijamii. Hivyo niwajulishe Watanzania kuwa taarifa hiyo ni ya uwongo na walioitoa wamefanya hivyo kwa maslahi wanayotajua wao."
​
SHETANI HANA RAFIKI,Ndugu Yericko Nyerere wewe si bora zaidi ya Polepole na Chonchori!

Hao wote walikuwa makada wa CCM wa kutupwa lakini wako wapi?,wale wale watu waliowadharau wakati wakila wali kwa uma ndo hao hao leo wanawalilia!

CCM wana kawaida ya kukutumia ili kufanikisha malengo yao ila baada ya hapo utakiona cha Moto!

Lakini pia ukiwa mwana jamii na mwanasiasa kijana,ni vema ukaacha kutumika kuwadhihaki wenzio,Mambo hubadirika ndani ya muda mfupi sana kuliko watu wanvyodhani!

Narudia tena,Mambo hubadirika sana
 
Back
Top Bottom