Je, ni kweli Jumuiya za Kimataifa zinaingilia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania?

Je, ni kweli Jumuiya za Kimataifa zinaingilia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kumekuwa na mijadala kutoka kwa watu mbalimbali hata humu JF kuwa mataifa ya nje na Jumuiya za nje zinaingilia Uchaguzi wetu, wengine wamefikia hatua ya kusema kuwa kuna baadhi ya wagombea wametumwa na ‘mabeberu’ kwa makubaliano fulani.

Kama kweli, Je, Jumuiya za kimataifa kama UN, EU, na mataifa makubwa kama USA, UK, zina uhalali gani na uchaguzi wetu. Nini hasa malengo yao. Kuna faida yeyote kwa nchi yetu. Kuna ushahidi wowote wa mtu anayetumiwa, nasisitiza ushahidi.

Concern yangu imechagizwa na trend ya matukio ya barua mfulizo kutoka kwenye Jumuiya hizo. Mfano wa barua hizo.

1. Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa UN, Michelle Bachelet.
''UN imekuwa ikipokea ripoti kuhusu ukamataji holela na kushikiliwa kwa wanaharakati, waandishi wa habari na wapinzani.

2. The US Defence Department “Pentagon” think tank warned Magufuli of political repression.

3. Congress Resolutions H. RES. 1120.

4. Robert Amsterdam and Partners LLP: An Open Letter to the Tanzania Police Force Regarding Attacks against Tundu Lissu.

5. An Open Letter to President Magufuli and Chief Justice Juma. By Robert Amsterdam.

Barua hizi na matamko haya pamoja na matukio mbalimbali ya NEC, ZEC na kutoka kwa wagombea hasa wa urais katika kipindi hiki, ndiyo yamenifanya niwe na wasiwasi na hatima ya Tanzania kabla na baada ya Uchaguzi wa mwaka huu, kwa sababu tangu nchi yetu ipate uhuru hatujawahi kuandikiwa resolutions za aina hiyo.

Nini kifanyike. Karibu tujadili.
 
Back
Top Bottom