Je, ni kweli kabisa Rais hafahamu chochote kuhusu haya ya utekeaji? Hiki ni kipimo kizuri

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,329
Reaction score
25,263
Wakuu,

Kumekuwa na member wengi ambao wanaona na kusema kwamba haya ya utekaji, torture na mauwaji, mh Rais hafahamu chochote na wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna hujuma dhidi yake.

Nadhani kuna mambo kadhaa anayoweza kuyafafanya kama ni kweli hafahamu chochote kuhusu yanayoendelea na kwamba anahujumiwa na hao watesi.

Mh Rais alisema atahakikisha uchunguzi unafanyika, na pia alijitolea kumlipia matibabu yule kijana Sativa ambaye aliitekwa na kuumizwa sana. Inaonekana aliponea kifo maana alipigwa risasi ya kichwa.

Kimsingi, kijana alitaja watu ambao ndiyo watakaokuwa incharge kwenye uchunguzi wowote utakaoendelea.

Kipimo kizuri kwa maoni yangu, ni kama atakubali uchunguzi ufanywe na chombo kama Scotland Yard.

Akikubali hilo, basi nitaamini ni kweli hafahamu lolote kuhusu hii operation ya utekaji, mateso na mauwaji, na kweli atakuwa anahujumiwa.

Endapo atakataa, hapo nitaamini kwamba anafahamu yote yanaoendelea na wala hakuna anayemhujumu kama wengi wa wale chawa wake wanavyotaka tuamini.Soma Pia:
 
siamini kwenye kuleta wapelelezi toka nchi nyengine!,wanaweza wakanusa jambo jengine na wakaamua walichukulie serious kutokana na interest zao,za matajiri wao ama serikali za nchi zao!.. msifikiri wale huwa wanakuja kwa swala moja tu never!.
 
Hakuna haja ya Scotland yard Bali a ateue tume ambayo haihusishi vyombo vya Dola hasa polisi.wateue wanasheria kutoka TLS,LHRC,jaji/wanasheria kutoka tume ya maadili na utawala Bora,na wanasheria kutoka vyama vya upinzani uone kama Hawa wapuuzi wanaoteka kama hawatafahamika.watekaji wanafahamika ispokuwa wanalindwa na serikali.
 
bila kuwa na wataalum wamaswala yakipelelezi wanaweza wasipate kitu au wakapata watu sio,upelelezi ni idara nyeti mkuu huteui tu watu hovyo ukatue mwanasheria akamuhoji mtuhumiwa na amsome psychology unajua psychology inavyochanganya na elimu zake babu!.. mbona mnaandika kama vile vitu rahisi sana!. basi kutakuwa hakuna haja yakuwa na wataalum hata mimi leo tufanye nimeshakuwa daktari njoo nikudunge sindano sasa...😂
 
Uhai wa Mtanganyika ni muhimu na WA thamani kuliko kitu chochote.

Waje tu hata kama watagundua jambo JENGINE
 
Sasa kama rais hafahamu
Boss wa tiss hafahamu
Igp hawafahamu
Spika hafahamu
Ma rpc hawafahamu
Huoni kama ni hatari

Ova
Ni hatari kubwa. Ndio maama pendekezo la kuwaomba Scotland Yard wafanye hii kazi likatolewa. Lakini utashangaa utaambiwa jeshi letu la polisi lina weledi litafanya uchunguzi kikamilifu.
Hili jeshi halijawahi kufanya upelelezi wa tukio lolote la aina hii likatoa majibu. Mfano, mbunge Tundu Lissu alishambuliwa akiwa eneo linalolindwa na jeshi hilo, huu ni mwaka wa saba hawajafanya lolote. No wonder watu (baadhi) wanahitimisha polisi ndio watuhumiwa wa kwanza.
 
Wakuu,

Kumekuwa na member wengi ambao wanaona na kusema kwamba haya ya utekaji, torture na mauwaji, mh Rais hafahamu chochote na wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna hukuka dhidi yake.

Nadhani kuna mambo kadhaa anayoweza kuyafafanya kama ni kweli hafahamu chochot kuhusu yanayoendelea na kwamba anahujumiwa na hao watesi.

Mh Rais alisema atahakikisha uchunguzi unafanyika, na pia alijitolea kumlipia matibabu yule kijana Sativa ambaye aliitekwa na kuumizwa sana. Inaonekana aliponea kifo maana alipigwa rızası ya kichwa.

Kimsingi, kijana alitaja watu ambao ndiyo watakaokuwa incharge kwenye uchunguzi wowote utakaoendelea.

Kipimo kizuri kwa maoni yangu, ni kama atakubali uchunguzi ufanywe na chombo kama Scotland Yard.

Akikubali hilo, basi nitaamini ni kweli hahahamu lolote na anahujumiwa.

Endapo atakataa, hapo nitaamini kwamba anafahamu yote yanaoendelea na wala hakuna anayemhujumu kama wengi wa wale chawa wake wanavyotaka tuamini.
Ukweli ni huu ndugu hakuna jambo linafanyika katika system Rais asijue mfano mdogo yule kijana aliye tekwa na kupigwa risasi ya kichwa na kutupwa mbuga ya katavi (SATIVA) moja ya watu walio mhoji kule centro ni afande MAFWELE na alimtambua kwa picha baada ya siku 20 na ni mtu anaye julikana mbona mpaka leo hakuna alicho fanuwa wala hakuna uchunguzi unao endelea …. Kwa ufupi sana hakuna chombo chochote cha nje kitaruhusiwa kuja kufanya uchunguzi kama utabisha nimekaa paleeeeeeeeeeeee
 
bila kuwa na wataalum wamaswala yakipelelezi wanaweza wasipate kitu au wakapata watu sio,upelelezi ni idara nyeti mkuu huteui tu watu hovyo ukatue mwanasheria akamuhoji mtuhumiwa na amsome psychology unajua psychology inavyochanganya na elimu zake babu!.. mbona mnaandika kama vile vitu rahisi sana!. basi kutakuwa hakuna haja yakuwa na wataalum hata mimi leo tufanye nimeshakuwa daktari njoo nikudunge sindano sasa...😂
Kupeleleza jambo siyo lazima uwe polisi.mtu yeyote mwenye akili timamu na anajua Sheria na taratibu za Nchi anawezakufanya hiyo kazi Kwa kuangalia namna ilivyovunjwa Sheria Kwa kuhoji mashahidi ambao wanashuhudia huo uhalifu Mfano huyo sativa na ndugu wa watu waliopotelewa na watu wao Kwa kutekwa pamoja na kuchunguza mawasiliano kwenye simu zao Kwa kushirikisha mitandao ya simu husika.
 
Wakuu,

Kumekuwa na member wengi ambao wanaona na kusema kwamba haya ya utekaji, torture na mauwaji, mh Rais hafahamu chochote na wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna hukuka dhidi yake.

Nadhani kuna mambo kadhaa anayoweza kuyafafanya kama ni kweli hafahamu chochot kuhusu yanayoendelea na kwamba anahujumiwa na hao watesi.

Mh Rais alisema atahakikisha uchunguzi unafanyika, na pia alijitolea kumlipia matibabu yule kijana Sativa ambaye aliitekwa na kuumizwa sana. Inaonekana aliponea kifo maana alipigwa rızası ya kichwa.

Kimsingi, kijana alitaja watu ambao ndiyo watakaokuwa incharge kwenye uchunguzi wowote utakaoendelea.

Kipimo kizuri kwa maoni yangu, ni kama atakubali uchunguzi ufanywe na chombo kama Scotland Yard.

Akikubali hilo, basi nitaamini ni kweli hahahamu lolote na anahujumiwa.

Endapo atakataa, hapo nitaamini kwamba anafahamu yote yanaoendelea na wala hakuna anayemhujumu kama wengi wa wale chawa wake wanavyotaka tuamini.
Huu ni uongo kabisa wote wanaelewa
 
Kupeleleza jambo siyo lazima uwe polisi.mtu yeyote mwenye akili timamu na anajua Sheria na taratibu za Nchi anawezakufanya hiyo kazi Kwa kuangalia namna ilivyovunjwa Sheria Kwa kuhoji mashahidi ambao wanashuhudia huo uhalifu Mfano huyo sativa na ndugu wa watu waliopotelewa na watu wao Kwa kutekwa pamoja na kuchunguza mawasiliano kwenye simu zao Kwa kushirikisha mitandao ya simu husika.
🤣🤣 wenye fani yao wanapita wanacheka hapa..
 
Hakuna haja ya Scotland yard Bali a ateue tume ambayo haihusishi vyombo vya Dola hasa polisi.wateue wanasheria kutoka TLS,LHRC,jaji/wanasheria kutoka tume ya maadili na utawala Bora,na wanasheria kutoka vyama vya upinzani uone kama Hawa wapuuzi wanaoteka kama hawatafahamika.watekaji wanafahamika ispokuwa wanalindwa na serikali.
Usipinge vitu usivokuwa na ujuzi navo bro,Norway kuna jamaa alimuuwa msomali alikuwa taxi driver, wakawaleta FBI mbona kila kitu kilikuwa wazi jamaa mzungu mbaguzi alipatikana,Na wao wana wataalam zaidi kuliko sisi.
 
Ukweli ni huu ndugu hakuna jambo linafanyika katika system Rais asijue mfano mdogo yule kijana aliye tekwa na kupigwa risasi ya kichwa na kutupwa mbuga ya katavi (SATIVA) moja ya watu walio mhoji kule centro ni afande MAFWELE na alimtambua kwa picha baada ya siku 20 na ni mtu anaye julikana mbona mpaka leo hakuna alicho fanuwa wala hakuna uchunguzi unao endelea …. Kwa ufupi sana hakuna chombo chochote cha nje kitaruhusiwa kuja kufanya uchunguzi kama utabisha nimekaa paleeeeeeeeeeeee
Sibishi mkuu. Ila nitaamini tu kuwa anafahamu kila kinachoendelea.
 
siamini kwenye kuleta wapelelezi toka nchi nyengine!,wanaweza wakanusa jambo jengine na wakaamua walichukulie serious kutokana na interest zao,za matajiri wao ama serikali za nchi zao!.. msifikiri wale huwa wanakuja kwa swala moja tu never!.
Tolea mfano hilo jambo jingine ambalo wanaweza wakanusa.
 
yapo maswala kibao ya uchumi na mali ambazo aidha serikali imezigundua na imeamua kuweka siri so,kwakuwa mmewapa mamlaka ya kufanya upelelezi wanaweza wakapata access yakunusa vitu kama hivyo!,kisa kimoja hunusa chengine dunia sasahivi inaumafia wa hatari kuhusu ujasusi wa kiuchumi.. hata wao wanaweza wasiifanyie kazi hiyo taarifa ila wakaiuza kwa wenye uwezo wao baadae mnaanza kusumbuliwa,ikitumika pesa vyema wenye tamaa wanauza kwa kisingizio cha uwekezaji halafu unakuwa hauleti tija kitaifa ukute ni mali ambayo inaweza kuhudumia taifa nyanja zote na chenchi ikabaki!..
ama mkiwa wabishi mnagombanishwa mtibuane waje wafanye mambo yao!.
 
siamini kwenye kuleta wapelelezi toka nchi nyengine!,wanaweza wakanusa jambo jengine na wakaamua walichukulie serious kutokana na interest zao,za matajiri wao ama serikali za nchi zao!.. msifikiri wale huwa wanakuja kwa swala moja tu never!.
Wazungu hakuna wasilolijua kuhusu sisi, hata nguo za ndani za viongozi wa nchi waliovaa leo watakua wanajua.

Internet ya kwao, twitter ya kwao, electronics gadgets zote nchini ni wao, computers wanazotumia ikulu ni zao.

Hivi we unawafahamu FBI na CIA au unawasikia?

Umeongea ni nonsense na upuuzi.
 
aiseee ushakosa hata tumaini mkuu! yaonyesha upo radhi kwa kila kitu ndo ulipofikia hapo
 
Acha kudanganya watu masuala ya usalama wa nchi, usalama wa nchi zetu hizi za kimasikini hadi vyoo vya watoto wa shule kwa msaada wa kina Billgate ndipo useme tuna usalama wankujificha mbele ya wazungu? Ambao kila kitu wanatawala wao, mifumo ya kibenki, internet, satellite n.k

Umeoandika hoja isio na mashiko ndio maana umeshindwa kujibu.
 
Back
Top Bottom