Wakuu,
Kumekuwa na member wengi ambao wanaona na kusema kwamba haya ya utekaji, torture na mauwaji, mh Rais hafahamu chochote na wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna hukuka dhidi yake.
Nadhani kuna mambo kadhaa anayoweza kuyafafanya kama ni kweli hafahamu chochot kuhusu yanayoendelea na kwamba anahujumiwa na hao watesi.
Mh Rais alisema atahakikisha uchunguzi unafanyika, na pia alijitolea kumlipia matibabu yule kijana Sativa ambaye aliitekwa na kuumizwa sana. Inaonekana aliponea kifo maana alipigwa rızası ya kichwa.
Kimsingi, kijana alitaja watu ambao ndiyo watakaokuwa incharge kwenye uchunguzi wowote utakaoendelea.
Kipimo kizuri kwa maoni yangu, ni kama atakubali uchunguzi ufanywe na chombo kama Scotland Yard.
Akikubali hilo, basi nitaamini ni kweli hahahamu lolote na anahujumiwa.
Endapo atakataa, hapo nitaamini kwamba anafahamu yote yanaoendelea na wala hakuna anayemhujumu kama wengi wa wale chawa wake wanavyotaka tuamini.
Soma Pia: