Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Kama haupo Ulipojiandikisha hupigi kura hata za Rais?

Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Kama haupo Ulipojiandikisha hupigi kura hata za Rais?

Mshangai

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2008
Posts
468
Reaction score
1,086
NEC watupatie elimu hii sawa sawa. Je, ni kweli kuwa bado nikiwa ndani ya Tanzania lakini nje ya kituo nilichojiandikisha siwezi kupiga kura ya Rais?

Kuhusu ubunge hiyo ni sawa, lakini kura ya Urais inashindikana nini wakati mataifa mengine wameweza hadi kupigia nje ya nchi?

Katika zama hizi za technolojia ya mawasiliano tunawezaje kunyima nafasi Raia ambao kwa sababu moja au nyingine hawapo mahali walipojiandikisha.
 
Sasa utapigaje kura sehemu ambayo hujajuandikisha? Kila kituo kina orodha ya wapiga kura, kwahiyo uwezi piga kura sehemu ambayo hakuna jina lako!

Hii inaondoa mwanya wa ninyi kusema mmeibiwa kura!
 
Nadhani sikupewa maelekezo yote hayo kwakuwa walijua Mimi ni ngemharibia Jiwe
Kwamba Kura yako moja ingemharibia huyo unaemuita jiwe?😂😂 Kwakweli miaisha yamewapa stress sana.Sasa sijui itakuwaje tukiongeza na mingine mitano.

Vijana jishughulisheni,hizi siasa haziatawasaidia chochote.Hebu fikiria mtu alieanza kuota ndoto Kama zako kuanzia multipartisim ianze mpaka Sasa atakuwa na umri gani? Hayo aliyoyaota kwa muda wote huo yametokea?

NB:Vijana mlioko kitaa,jobless acheni kuishi kwenye ndoto za wenzenu. Ulizeni waliofanikiwa katika mazingira Kama yenu walifanyeje.Huu ushabiki huwa ni wa kipindi kifupi sana.
 
Nadhani sikupewa maelekezo yote hayo kwakuwa walijua Mimi ni ngemharibia Jiwe

Sio swala la kutopewa maelekezo ni swala la wewe kuwa mjing mjinga ndio maana vitu vidogo kama hivi hadi leo hamvijui halafu mnawadanganya watu mtashinda uchaguzi hahahaha! Wajinga kama ninyi wako wengi sana humu wanashangilia tuu lakini hawajui kama hawewezi kupiga kura popote.
 
NEC watupatie elimu hii sawa sawa. Jee ni kweli kuwa bado nikiwa ndani ya Tanzania lakini nje ya kituo nilichojiandikisha siwezi kupiga kura ya Rais?

Kuhusu ubunge hiyo ni sawa, lakini kura ya Urais inashindikana nini wakati mataifa mengine wameweza hadi kupigia nje ya nchi?

Katika zama hizi za technolojia ya mawasiliano tunawezaje kunyima nafasi Raia ambao kwa sababu moja au nyingine hawapo mahali walipojiandikisha
Kupigia kura mahali usipojiandikisha kutatoa mwanya kwa CCM kuchomekea mamluki pamoja na kura za maruhani. Tuache hali iendelee hivyo hivyo ili kuwadhibiti hawa fisi.
 
Sasa utapigaje kura sehemu ambayo hujajuandikisha? Kila kituo kina orodha ya wapiga kura ...kwahiyo uwezi piga kura sehemu ambayo hakuna jina lako!

Hii inaondoa mwanya wa ninyi kusema mmeibiwa kura....!
Unatumia BVR kuandikisha wapiga kura kisha mtu hawezi kupiga kura kituo ambacho hajajiandikishia, huo sio upumbavu wa kiwango cha lami?

Kulikuwa na sababu gani kutumia gharama kununua devices na software pamoja na kutrain watu wakati kiuhalisia tume ina operate manually?

Kuliko kufuja kodi zetu, wangetumia daftari za mia mbili kwenye vituo kuandikisha wapiga kura kisha hizo fedha tukaelekeza maeneo mengine.
 
Kwamba Kura yako moja ingemharibia huyo unaemuita jiwe?😂😂 Kwakweli miaisha yamewapa stress sana.Sasa sijui itakuwaje tukiongeza na mingine mitano.

Vijana jishughulisheni,hizi siasa haziatawasaidia chochote.Hebu fikiria mtu alieanza kuota ndoto Kama zako kuanzia multipartisim ianze mpaka Sasa atakuwa na umri gani? Hayo aliyoyaota kwa muda wote huo yametokea?

NB:Vijana mlioko kitaa,jobless acheni kuishi kwenye ndoto za wenzenu. Ulizeni waliofanikiwa katika mazingira Kama yenu walifanyeje.Huu ushabiki huwa ni wa kipindi kifupi sana.
Ulipaswa kupewa fomu ujaze then upige kura moja ya Uraisi.
Nadhani sikupewa maelekezo yote hayo kwakuwa walijua Mimi ni ngemharibia Jiwe

Mimi na wewe nani jobless?

Nataka nijaze form za Forbes ndio next year tutaheshimiana
 
kunakuwaga kipind cha kuhakiki taarifa za mpiga kura ilo linawasaidia wale watakao hama kituo ama mkoa kurekebisha taarifa zao sasa kama huo Muda ulifka na haukuchukua hatua yoyote ilo ni kosa lako.
 
Mtoa mada ana hoja ya msingi watu sio mawe kuna madereva na kuna dharura movement hazikwepeki,sasa enzi hizi za technology hiyo kitu inawezekana
 
Nadhani sikupewa maelekezo yote hayo kwakuwa walijua Mimi ni ngemharibia Jiwe

Mimi na wewe nani jobless?

Nataka nijaze form za Forbes ndio next year tutaheshimiana
Form za nini?😂😂 Wewe hata TIN number huna.Acha kuwatafutia wenzako ulaji kisiasa,pambana kabla umri haujakutupa mkono.

NB:Nakushauri tu kijana,ya sisi CCM hutayaweza kamwe.
 
Vijana jishughulisheni,hizi siasa haziatawasaidia chochote.Hebu fikiria mtu alieanza kuota ndoto Kama zako kuanzia multipartisim ianze mpaka Sasa atakuwa na umri gani? Hayo aliyoyaota kwa muda wote huo yametokea?

Mkuu nadhani huelewi hata maana ya siasa ndio maana unabwatuka hivyo.

Mtu anayedhani anaweza kuwa na maisha nje ya siasa ni mtu ambaye bado hajajitambua kabisa. Siasa/Wanasiasa ndio wanaamua maisha yaende vipi.

Umewahi kuwaza kuwa hata uwe na mafanikio vipi, utajenga shule yako ili wanao wapate elimu? Utajenga hospitali ili utibiwe? Utajenga barabara ili usafiri?

Leo kuna watu walipambana kama unavyo shauri lakini kutokana na siasa mbovu, nyumba walizo jenga zimebomolewa hawana hata pa kuishi. Wengine wamefilisiwa mitaji yao kwa siasa mbovu.

Wengine wamekufa sababu ya siasa mbovu na pengine kwenye uhai wao walikuwa na fikra kama zako kuwa siasa haiwahusu hivyo hawakushiriki kuchagua viongozi wazuri wakawaachia watu wakawawekea watu wa hovyo.
 
Ili kuwa na hakika ya kuwapigia wagombea unawataka inakulazimu uwe mahali ulipojiandikisha wakati ulipojisajili katika daftari la wapiga kura, Haya maelezo mengine ya kujaza fomu maalum siku ya kupiga kura yapo lakini ukifika katika kituo cha kupiga kura unaweza usipige kura kwa sababu jina lako halipo katika hicho kituo.
 
Unatumia BVR kuandikisha wapiga kura kisha mtu hawezi kupiga kura kituo ambacho hajajiandikishia, huo sio upumbavu wa kiwango cha lami?

Kulikuwa na sababu gani kutumia gharama kununua devices na software pamoja na kutrain watu wakati kiuhalisia tume ina operate manually?

Kuliko kufuja kodi zetu, wangetumia daftari za mia mbili kwenye vituo kuandikisha wapiga kura kisha hizo fedha tukaelekeza maeneo mengine.
NEC wanao uwezo wa kuhesabu kura zinazopigwa katika kituo chochote. Chadema ndio wanakataa utaratibu huo usitumike. Kwahiyo usiwalaumu NEC, walaumu Chadema.
Wasingesikilizwa, mngelalamika kuwa kuna uchakachuaji!
 
Back
Top Bottom