Hayajapita majuma matatu tangu Mwenyekiti wa zamani wa Mamlaka ya kudhibiti matumizi ya pombe na dawa za kulevya( NACADA) John Mututho, kutoa madai mazito kuwa vodka zinazouzwa nchini Kenya hazitengenezwi kwa viwango halisi vya kimataifa na kwamba zilizoko hutumia ethanol ya viwandani.
Ni madai mazito yanayoendelea kufanya wengi kujikuna kichwa hasa wikendi zinapoingia na mtu unatoka na washikaji zako kuangalia mpira labda.
Lakini swali ni:
Je, madai haya ya Mututho yamethibitishwa rasmi na maabara za Serikali au mamlaka za ubora? Mpaka kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS wala kutoka kwa mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA au mamlaka nyingine za udhibiti kuwa "hakuna vodka halisi Kenya."
Hatahiyo Serikali inaendelea kufanya operesheni nyingi dhidi ya viwanda vya pombe ghushi, jambo linaloonyesha kuwa changamoto ya bidhaa feki ipo.
Aidha leo Jumapili September 20 Meneja wa Kanda ya Magharibi wa NACADA, Sarah Koske, amezitaka jamii kuchukua hatua kukabiliana na uraibu wa pombe miongoni mwa vijana na kudhibiti madhara yanayotokana na matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
Baadhi ya wakazi wa Kisumu vile vile, pamoja na wanaharakati wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya, walishiriki katika Maandamano ya Uhamasishaji kuhusu Kinga dhidi ya Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya, yaliyoandaliwa na Blue Cross, Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni dhidi ya Pombe na Matumizi ya Dawa za Kulevya (NACADA), pamoja na mashirika mengine washirika.
Matembezi hayo yalilenga kuongeza uelewa kuhusu changamoto zinazoongezeka za kiafya, kiuchumi na kijamii zinazohusishwa na matumizi ya dawa za kulevya, hususan miongoni mwa vijana nchini.
(Picha za walioshiriki matembezi: courtesy of Clinton Ambujo)
Watumiaji wanawezaje kujilinda?
Je, umewahi kukutana na pombe unayoshuku kuwa ilikuwa ghushi?
Unadhani mamlaka zinafanya vya kutosha kudhibiti bidhaa feki sokoni?
Ni hatua gani zingechukuliwa kuimarisha usalama wa watumiaji?

- Nunua kutoka maduka yanayoaminika.
- Hakiki stika za KRA kwa kutumia KRA Soma Label kwenye kifuniko cha pombe yako. Kumbuka KRA hutumia mifumo ya udhibiti kama stika za ushuru kusaidia kutambua bidhaa halali.
- Kuwa makini na bei ambazo ni za chini kupita kiasi.