POTOSHI Je, ni kweli Kondoo ana viumbe kama funza kwenye ubongo wake wanaomchochea kupigana au kupambana na radi?

POTOSHI Je, ni kweli Kondoo ana viumbe kama funza kwenye ubongo wake wanaomchochea kupigana au kupambana na radi?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
1784547764399.png

1784547908060.png
 
Tunachokijua
Madai

Inadaiwa Kondoo wana wadudu kama funza kwenye ubongo ambao hata radi ikipiga funza hao huchachamaa na kusababisha kondoo kutapatapa. Pia inaelezwa funza hao wakichachamaa wakati mwingine husababisha kondoo kutaka kupigana.

Je, madai haya yana uhalisia kiasi gani au kuna upotoshaji?

Mtaalam wa Kilimo na Mifugo Jordan Majaliwa, anaeleza kuwa jambo hilo ni upotoshaji kwani hakuna uhusiano wowote wa kisayansi kati ya radi na uwepo au utendaji wa funza/minyoo kwenye ubongo wa kondoo.

Mtaalamu huyu anakiri kuwa ni kweli kwamba kondoo hupatwa na ugonjwa unaosababishwa na aina ya minyoo/funza wanaokaa kwenye ubongo (ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama Cerebral Coenurosis au Gid / Staggers).

Kuhusu radi inapopiga au kunapokuwa na mshtuko mkubwa wa sauti, kondoo aliye na mshituko au ugonjwa huu kuwa na tabia ya kutapatapa, kuzunguka-zunguka, kupoteza mwelekeo, au kuinamisha kichwa chini/ukutani. Huu ni mshtuko tu na si kwamba radi inasababisha funza hao kuchachamaa au kupigana.

Tabia za Ugonjwa na Kondoo Wanaoadhirika

Dalili Kuu (Clinical Signs): Kondoo mwenye ugonjwa huu huonyesha dalili za kuzunguka-zunguka (circling), kutapatapa, na kupoteza uratibu wa kawaida wa mwili.

Ugonjwa huu unawapata zaidi kondoo wakubwa kwani ni nadra sana kupata kondoo wadogo (young sheep) wakiwa na changamoto hii.

Mtaalamu anaeleza kuwa ugonjwa huu unatibika kwa kutoa matibabu na sindano stahiki pindi dalili za kitaalamu zinapobainika.

Madai kwamba radi inawasha au kuchachamaza funza kichwani mwa kondoo si ya kweli. Ni mshtuko wa sauti au mazingira unaofanya kondoo mwenye ugonjwa wa minyoo ya ubongo kuonyesha dalili za kutapatapa na kupoteza mwelekeo.​
Sio kweli
Soma kitu kinaitwa nasal boots in sheep's
 
Back
Top Bottom