Je, ni kweli kuna genge linataka kukwamisha juhudi za Rais?

Je, ni kweli kuna genge linataka kukwamisha juhudi za Rais?

Tangu amechukua nafasi ya uongozi baadhi ya Watanzania tuliona mbali tukamshauri kuondoa wale watendaji waliokuwa karibu zaidi na serikali ya mwendazake na kuchagua watu wengine ambao watakuwa wanamtii hasa pale anapotoa maelekezo fulani yafanyike ila mh. Raisi hakuzingatia ushauri huo leo amekuja kujua .
Rais alikuwa sahihi.....ni TIMING tu ....
 
FB_IMG_16307140795615105.jpg
 
Hakuna uhalisia wowote ni kujaribu kukwepa majukumu yako. Wewe kama ndo kiongozi mkuu wa serikali, Rais, amri jeshi mkuu, mwenyekiti wa CCM taifa unashindwa je kusambaratisha hayo makundi kama unayafaham yapo?
Akhsante sana ndugu MkamaP ,umeandika hali halisi.

Una vyombo vyote vya kukupa taarifa kuwa unahujumiwa na kuzuia hujuma,unashindwajee kuchukua hatua?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Angejiuliza kwanza yeye mwenyewe, kwa nini inasemwa hivyo juu yake au serikali yake; na sio lazima wanaosema hivyo wawe wapo ndani ya serikali yake au wawe ndani ya genge.

Haya yanasemwa na watu hata wasiokuwa na uhusiiano wowote na awamu ya tano. Ajiulize kwa nini isemwe hivyo juu ya serikali yake.

Kuna mambo gani ameyafanya yanayoonyesha yeye mwenyewe na genge la watu anaowateua kuwa hawaaminiki?
Asikimbilie kujihami kwa vitendoi vya awamu nyingine, atazame matendo yake na yanayofanyika ndani ya serikali yake kwa sasa hivi.
 
Hakuna uhalisia wowote ni kujaribu kukwepa majukumu yako. Wewe kama ndo kiongozi mkuu wa serikali, Rais, amri jeshi mkuu, mwenyekiti wa CCM taifa unashindwa je kusambaratisha hayo makundi kama unayafaham yapo?
Nadhani mama anajaribu kukwepa ukweli wa mambo hapa, kwa ku'deflect' tatizo kwa wengine.

Yeye analaumu "genge lililomo serikalini" likilalamikia serikali yake. Je, amejaribu kusikiliza na huko kwingine ambako siyo kwenye magenge wanasemaje kuhusu mwenendo wa serikali yake?

Hisia za wananchi wa kawaida zikoje, wanasemaje?
 
Back
Top Bottom