Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Kuna threads hapa zimepostiwa juzi zinauliza kulikoni mawaziri na raisi wao wamekimbilia Dodoma?
Kumbe ishu ni hii Corona ya mwenzao
 
Timu yote iliyoambatana na Kabudi akiwemo yule waziri wa Zanzibar wanaugua Corona kali sana . Nasema kali sana kwasababu ni tofauti kabisa na hii ya wabongo. Yule wa Zanzibar aligoma kutolewa pia hospital ila katolewa kwa nguvu na bado hali yake ni tete, kapelekwa kambini huko. Sasa mkitaka kujua ukali wa Corona mungewaona hawa waliotokea Italy haki ya Mungu wenyewe mtajiweka ndani. Mtu anapumua kama king'ora cha gari ya ambulance! Hapana huu ugonjwa una shetani lake wallahi
 
Tuendelee kuwaombea
 
Huyo waziri Mzanzibari inaonekana hata akifa atakataa kuzikwa kaburini sababu ya "hadhi" yake
 
Nilisikia hata Faulk Khaarim akilalamika kuwa huko Zanzibar W Akitoa taarifa hawataki waulizwe maswali kama mgonjwa ni wa bara ama visiwani huu ushamba wa viongozi wa Tanzania utatugharimu. Mwana wa Malikia kajitaja , Waziri mkuu wa uingereza kajitaja sasa hao wetu ni wakina nani wasitoe ushirikiano. Hatujawaambia wataje majina hata kidogo
 
Ninakuheshimu sana ila post hii hata kama ina ukweli mtupu, hukuiandika vizuri kwani umeiweka kishabiki zaidi kuliko kuifanya iwe informative na objective tu. Kama mtu kaambukizwa tu, hakuna tatizo kutangaza na kuweka wazi kuwa hatakutana na watu kwa wiki mbili kwa sababu hiyo, ila iwapo mgonjwa ni mahututi yuko ICU hilo linabaki swala la mgonjwa mwenywe, familia yake na pamoja daktari wake.

Matangazo ya maambukizi kama ya ugonjwa huu ni lazima yadhibitiwe ili kupunguza taharuki kwenye jamii. Serikali kutotangaza siyo lazima kuwa wanaficha. huenda muda wa kutangaza haujafika. Tulipokuwa na kipindupindu, bado matangazo hayakuwa ya kiholea kila mtu akijitajia mambo yake; yote yalitolewa na serikali. Hata marekani data zote za maambukizi leo zinatoka serikalini, siyo kila mtu anajitanganzia bali zinatangwzwa na ofisi maalum tu.
 
Pascal Mayalla nakushauri futa huu uzi. Kama ulipokonyoka ktk line ya akina Kabendera hapa utanasa. Ni ushauri tuu maana umetafutiwa target muda mrefu.
Acheni kutisha watu. Kosa la Pascal ni nini? Si ameuliza? Si ametahadharisha? Kama siyo kweli, kinachotakiwa ni kukanusha na kuueleza ukweli.

Tukiwa waoga, tena kwenye mambo ya msingi, na wakati hakuna sheria iliyovunjwa, wanaotaka kutisha watu kwa dhamira ovo, wataendelea kufanya hivyo. Huenda hata Rais hajaambiwa juu ya ukaidi uliofanywa na huyo mgonjwa, si wakati wote Rais huambiwa kila kitu. Lakini habari kama hizi zinapokuwa wazi, atafuatilia. Na kama yanayoelezwa ni kweli, basi yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa amri, na huyo mteule wake akatii.

Nina hakika kama hayo maambukizi, hata yangempata Rais, angejitenga. Sasa huyo kwa nini awe mkaidi?
 
Mkuu Mimi ni ccm damu lakini kwa huu upuuzi wanaotufanyia kwa kweli haifai,hawataki kutupatia updates za ugonjwa kwa lengo la kulinda utalii ili khali huku raia wanaangamia,ikiwa ugonjwa huu utauwa raia wa Tanzania wengi itakuwa ni muda muafaka wa raia kuiadhibu ccm kwa damu na jasho
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sijaingia ndani kujua ukweli au uzushi wa bandiko. Nimempa tahadhari tu kama member mwenzangu wa JF baas.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…