PureView zeiss
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 10,786
- 35,916
Kuna threads hapa zimepostiwa juzi zinauliza kulikoni mawaziri na raisi wao wamekimbilia Dodoma?
Kumbe ishu ni hii Corona ya mwenzao
Kumbe ishu ni hii Corona ya mwenzao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuendelee kuwaombeaTimu yote iliyoambatana na Kabudi akiwemo yule waziri wa Zanzibar wanaugua Corona kali sana . Nasema kali sana kwasababu ni tofauti kabisa na hii ya wabongo. Yule wa Zanzibar aligoma kutolewa pia hospital ila katolewa kwa nguvu na bado hali yake ni tete, kapelekwa kambini huko. Sasa mkitaka kujua ukali wa Corona mungewaona hawa waliotokea Italy haki ya Mungu wenyewe mtajiweka ndani. Mtu anapumua kama king'ora cha gari ya ambulance! Hapana huu ugonjwa una shetani lake wallahi
Tunasubiri Mamu wa Dar atangaze ili kuwaokoa wananchi wa Dar!Wakati mwingine uwe serious na issue zenye public interest. Bahati yako niko Chato ningekuibukia hapo ulipo ili unieleze vizuri upupu wako huu!
Corona imetinga Dodoma kaamua kupakimbia!😆😆😆😆Mkulu mwenyewe ktimkia Chato hataki lawama za kuambiwa mbona hukuja kunisabahi
Kwani wewe umejibu hapa inakuhusu nini!Kwani akiugua korona wewe inakuhusu nini
Tunasubiri Makonda atangaze ili kuwaokoa wananchi wa Dar!Mkuu Mayala safi sana umefanya kama Makonda alivyomuumbua Mbowe juzi
Sent using Jamii Forums mobile app
Ninakuheshimu sana ila post hii hata kama ina ukweli mtupu, hukuiandika vizuri kwani umeiweka kishabiki zaidi kuliko kuifanya iwe informative na objective tu. Kama mtu kaambukizwa tu, hakuna tatizo kutangaza na kuweka wazi kuwa hatakutana na watu kwa wiki mbili kwa sababu hiyo, ila iwapo mgonjwa ni mahututi yuko ICU hilo linabaki swala la mgonjwa mwenywe, familia yake na pamoja daktari wake.Wanabodi,
Naomba kuanza na Angalizo: Mamlaka pekee za kutangaza status report ya ugonjwa wa Corona kwa Tanzania ni
Hivi wajameni hii siyo taarifa ya update ya Corona, hili ni swali nimeuliza na alama kabisa ya kuuliza! Mimi mwenzenu kazi yangu ni kuuliza tuu maswali, na kuna swali niliwahi kuuliza, hadi nikaitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge, kuwa nimetoa statement, kumbe sikutoa statement yoyote bali nimeulizwa swali tu, hivyo bandiko hili nalo ni swali tu lenye alama ya kuuliza hii? nisije nikaitwa popote kuulizwa kuwa nimetoa statement yoyote, unless kwenye janga hili la Corona, hata sisi waandishi haturuhusiwi kuuliza chochote, hata ukisikia chochote kinachohatarisha usalama wa taifa letu tunyamaze tuu tukisubiria hadi hao wasemaji 4 waseme, wasiposema, tupotezee huku tunateketea?.
- Rais wa JMT
- Waziri Mkuu
- Waziri wa Afya
- Msemaji Mkuu wa Serikali
Kufuatia janga la Corona, tunahimizwa tusitangaze taarifa yoyote bila kuipokea kutoka Vyanzo rasmi vya kiserikali.
Lakini inapotokea wewe ni mwandishi wa habari makini na Mzalendo unao jua wajibu wako kama mwanahabari na wajibu wako kwa taifa lako, ukipokea habari kutoka chanzo ambacho wewe unakiamini, na ukathibitishiwa kuwa serikali inajua ila imenyamaza, kwa vile kunyamaza huko kunaweza kutusababishia majanga, hiyo kuitangaza taarifa hiyo ili serikali ichukuwe hatua stahiki ndio uzalendo wa kweli kwa taifa lako.
Mimi licha ya kuwa ni mwana habari, pia nimebahatika kufuta tongo tongo za sheria, hivyo, ili ku tie in all loose ends kunizuia nisitwe popote kuwajibishwa kisheria, naitoa taarifa bila majina, sijasema ni Waziri gani, au waziri wa wapi, hii ili kuisaidia serikali yetu ya JMT, kutimiza wajibu wake wa kuwalinda Watanzania dhidi ya maambukizi ya Corona huku nikiheshimu haki zote za the right to privacy.
Nimepokea taarifa hii kutoka very reliable source.
... jina limehifadhiwa (Waziri wa ...) ashukiwa kuugua CORONA.
************************************************************************
Waziri wa... ambaye alikuwa safarini akitua nchini kutokea London (Uingereza 🇬🇧) ambapo safari yake ilianzia Italy 🇮🇹 kisha kurejea wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya ... akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA.
Dr. Mkuu wa Hospitali ya ... baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya ... akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Corona, itakuwa ni aibu kwake na kumdhalilisha!.
Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika... Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA 🦠
Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda , kituo Maalum cha wagonjws wa Corona, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya Italy kisha kupitia London kurejea Tanzania na homa kali!
Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya hiyo alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake.
Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali hiyo pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine.
Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Watanzaia wote!... Ameitaka serikali kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya hiyo haraka kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari!
Mwisho.
My Take.
Kwa vile Corona ni issue za kitabibu, sio lazima kila anayeugua mafua makali ni Corona, inawezeka Waziri ana homa tuu ya kawaida na mafua ya kawaida lakini sio Corona, kama madaktari wanasema sio Corona then sio Corona!.
Lakini kama ni Corona,
Natoa Wito, Only The Truth & Transparency ndio The Only Way Out Kushinda Vita Hii. Kama Waziri Anaugua Corona, His/Her Rights To Privacy Be Upheld kwa kutokutajwa kwa jina wala wizara yake, ila Asipewe Any Preferential Treamement Kwasababu ni Waziri, Kama Ameugua Corona, Msifiche Waziri Wetu Kuugua Corona, Ugonjwa wa Corona sio ugonjwa wa aibu kusema tuufanye siri, Unaficha Nini?!. Marais wa dunia wame test positive na wametangaza, hadi mfalme ametangaza ndio itakuwa waziri?.
Kama ni kweli kuna Waziri anaugua Corona halfu tunaficha kwasababu yeye ni Waziri, Naomba kutoa angalizo la Kisa Cha Mficha Maradhi, nini huwa kinatokea ambacho Kitamuumbua. Naomba tusifike huko!
NB. Naombeni tusianze kupiga ramli chonganishi kumjua ni waziri gani, " umdhanie ndiye, siye!". Inawezekana ikawa ni jamaa mmoja jina lake Waziri!
I wish you Saturday night njema.
Paskali
Acheni kutisha watu. Kosa la Pascal ni nini? Si ameuliza? Si ametahadharisha? Kama siyo kweli, kinachotakiwa ni kukanusha na kuueleza ukweli.Pascal Mayalla nakushauri futa huu uzi. Kama ulipokonyoka ktk line ya akina Kabendera hapa utanasa. Ni ushauri tuu maana umetafutiwa target muda mrefu.
Zanzibar wako very objective kwenye reporting ya huu ugonjwa.
North Korea na sisi tofauti hamna.
Ina kera sana kuwa mnayaweka maisha ya watu wasio na hatia hatarini kwa kutanguliza maslahi yenu mbele.
Kwamba ni sababu za kiuchumi ni utalii utaharibika, you must be joking.
Ndiyo maana mnatuletea hadithi za uchaguzi mkuu.
Fumbo fumbieni wajinga.
Acheni kutisha watu. Kosa la Pascal ni nini? Si ameuliza? Si ametahadharisha? Kama siyo kweli, kinachotakiwa ni kukanusha na kuueleza ukweli.
Tukiwa waoga, tena kwenye mambo ya msingi, na wakati hakuna sheria iliyovunjwa, wanaotaka kutisha watu kwa dhamira ovo, wataendelea kufanya hivyo. Huenda hata Rais hajaambiwa juu ya ukaidi uliofanywa na huyo mgonjwa, si wakati wote Rais huambiwa kila kitu. Lakini habari kama hizi zinapokuwa wazi, atafuatilia. Na kama yanayoelezwa ni kweli, basi yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa amri, na huyo mteule wake akatii.
Nina hakika kama hayo maambukizi, hata yangempata Rais, angejitenga. Sasa huyo kwa nini awe mkaidi?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huyo waziri Mzanzibari inaonekana hata akifa atakataa kuzikwa kaburini sababu ya "hadhi" yake
Ndo matope ya watanzania haya, badala ya kutia moyo unaogofya mtu ili iweje.Pascal Mayalla nakushauri futa huu uzi. Kama ulipokonyoka ktk line ya akina Kabendera hapa utanasa. Ni ushauri tuu maana umetafutiwa target muda mrefu.
Punguza jazba za kike.Idiot comment ever!