Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Leo Mayalla umeandika kitu kizuri sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Update
Wanabodi, hii sasa sio tetesi tena, leo imethibitishwa rasmi Bungeni Dodoma, kuwa ni kweli kuna Waziri aliugua Corona na akagoma kwenda kutibiwa kwenye hospitali maalum iliyotengwa na badala yake akalazimisha kutibiwa hospital ya kawaida.

Serikali ilipopata taarifa ilituma watu wake na Waziri huyo alihamishwa kikuku na kuhamishiwa eneo rasmi lililotengwa, sasa anatibiwa huko na anaendelea vizuri.

Uthibitisho huu umetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya ofisi yake, katika hotuba iliyotangazwa live, mubashara kupitia TBC.

Waziri Mkuu amevishukuru sana vyombo vya habari kwa kutangaza habari kama hizi, ambazo zimeisaidia serikali kujua na kuchukua hatua.

JF ndicho chombo pekee rasmi cha habari kwa hapa nchini kuitangaza habari hii hivyo kuiwezesha serikali kuchukua hatua stahiki.

Nami niliyewaletea taarifa hii, naomba kumshukuru sana kwa dhati yule mshirika wangu muhabarishaji kutoka Zanzibar ambaye ni binti mrembo wa Kizanzibari anayejiheshimu na mimi namheshimu sana, Asante sana mwananahabari binti mwanamke shujaa wa Kizanzibari.

Kwa heshima ya mhe. Waziri na kwa kuzingatia maadili ya kidakitari ya kitu kinachoitwa " the confidentiality clause" cha kuficha siri ya mgonjwa kati ya dakitari na mgonjwa, na kwa kutumia kipengele cha " the right to privacy" kwa sisi waandishi kutuingilia faragha za watu, Waziri Mkuu hakulitaja jina la Waziri huyo, na mimi hapa naomba nisilitaje jina la Waziri huyo na kukuomba hata wewe, hata kama unalijua jina la Waziri huyu, tusilitaje.

Information is power, hongera kwa wewe mwana jf to be the first to know, na ukiwa na taarifa yoyote kama hii ambayo italisaidia taifa, usisite kuileta humu jf.
Nawatakia siku njema.

Paskali
 

Sasa wewe jina lako sahihi ni lipi hapo? Pascal au Paskali?
 

Kwa nini unaogopa hadi sasa kumtaja jina lake, ilhali limeshatajwa bungeni. Sema tu ni Salama Abutallib waziri wa madini Zanzibar
 
Mbunge wa CUF amchongea waziri wa Zanzibar kwa Waziri Mkuu
Mbunge wa Konde Nchini Tanzania (CUF) Khatib Said Haji ameiomba Serikali kumchukulia hatua Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib aliyekataa kukaa kwenye karantini na kusababisha maambukizi kwa watu wawili kwenye familia yake.

Akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 amesema matokeo ya hilo nyumbani kwake kuna watu wawili amewaambukiza na huko hospitali haijulikani matokeo yake nini.“Ndani ya siku tatu ameng’ang’ana kukaa hospitali ya Mnazi Mmoja matokeo yake akatolewa kwa nguvu baada ya kuona jambo hili limekuwa kubwa sana. Baada ya malalamiko makubwa ndio alikubali kuwekwa kwenye karantini,”amesema.Amesema alifanya hivyo kwa sababu ya kiburi cha madaraka yake na kumpongeza makamu wa pilli wa Rais Zanzibar kwa kukubali kukaa karantini alipotoka nje ya nchi bila kulazimishwa.“Huu ndio utu, huu ndio ubinadamu leo waziri huyu ni nani anayekataa uamuzi wa Serikali hata uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Hatuwezi kumchekea mtu mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu ni waziri ulichukulie hatua haraka. Leo hii baada ya kiburi kingine kuna mtu mwingine ni daktari anaitwa Hafidh hadi leo ameng'ang'ana pale Hospitali ya Mnazi mmoja kwa sababu ana unasaba wa kiukubwa.”“Uheshimiwa wake ni kwa sababu ana uhai anapumua dakika moja akifumba macho anakuwa marehemu. Taharuki iliyopo pale Mnazi mmoja baada ya matukio hayo ni kubwa. Nataka mheshimiwa ufuatilie kama huyu daktari bado yupo,”amesema.Amesema kauli anazozitoa katika mtandao ya jamii ni utasema hakuna yoyote anayeweza kumfanya lolote haya madhara yakianza mahali pamoja yanaenea.
 
Sasa wewe jina lako sahihi ni lipi hapo? Pascal au Paskali?
Jina la Paskali ni mtu aliyezaliwa siku ya Pasaka.
Akiwa mwanaume ni Paskali akiwa mwanamke ni Paskalia, Paskalina, Paskazia.
Kiitalina wanaandika Paschal, Kifaransa, Pasco, Kiingereza Pascal na Kiswahili ni Paskali
Lugha nyingine ni Pasqwa, Pascoe, Pascale, Pascalle, Paschal, Paskal, Pashk, Paschalis, Pascaline, Pasquale, Pascual, Pascoe, Pasco.

Jina langu ninalotumia sasa at the age of 50+ ni Paskali. At 60 nitaanguliza Mzee Paskali.
Nilipojiunga JF nilikuwa kijana nilikuwa Pasco.
Jina rasmi linavyo andikwa ni Pascal

P
 
Mkuu Michael Makene, asante nimekisikia, na karibu mitaa hii.
P
 
Kwa nini unaogopa hadi sasa kumtaja jina lake, ilhali limeshatajwa bungeni. Sema tu ni...waziri wa ... Zanzibar
Sheria ya right to privacy inataka mtu ajitaje mwenyewe, na sio kutajwa na wengine. Hata kule kutajwa anatajwa Waziri tuu bila kutajwa jina lake.
P
 
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P
 
Hii nimeipenda onghwise [emoji120][emoji122]. Umelifanyia utafiti jina lako. Wengine mambo haya hatuyawezi sijui ni uvivu ?!

Odhis *
 
Sheria ya right to privacy inataka mtu ajitaje mwenyewe, na sio kutajwa na wengine. Hata kule kutajwa anatajwa Waziri tuu bila kutajwa jina lake.
P

Hivi right of privacy haina kikomo? Huwezi kumtaja mwizi mpaka ajitaje mwenyewe? Right of privacy inamlinda hata anaevunja sheria au kuhatarisha maisha ya wenzake? Mie nahisi kuna right of privacy kuna limit zake. Pia kama ukisikiliza vizuri yule mbunge alimtaja jina waziri anaehusika, na kwa ninavyofahamu kuwa sheria za mabunge duniani ni kuwa wakati mbunge au mwakilishi analindwa na sheria zinazomruhusu kumtaja mtu yeyete yule anaetuhumiwa kwa lolote lile, mtuhumiwa anapokwisha kutajwa bungeni, huwa right of privacy imekwisha. Au Tanzania sheria za right of privacy ziko vyengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…