Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 52,160
- 48,974
Huu ugonjwa hauangalii cheo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pascal Mayalla nakushauri futa huu uzi. Kama ulipokonyoka ktk line ya akina Kabendera hapa utanasa. Ni ushauri tuu maana umetafutiwa target muda mrefu.
Somo haliwezi kuingia kirahisi kwa naibu raisMakonda alishaambiwa na Ummy
Aache kuropoka majini ya watu ovyo. Nadhani somo limemuingia
Wanabodi,
Naomba kuanza na Angalizo: Mamlaka pekee za kutangaza status report ya ugonjwa wa Corona kwa Tanzania ni
Hivi wajameni hii siyo taarifa ya status ya ugonjwa wa Corona na wala sio update ya Corona, hili ni angalizo la swali nimeuliza na alama kabisa ya kuuliza! Mimi mwenzenu kazi yangu ni kuuliza tuu maswali, na kuna swali niliwahi kuuliza, hadi nikaitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge, kuwa nimetoa statement, kumbe sikutoa statement yoyote bali nimeulizwa swali tu, hivyo bandiko hili nalo ni swali tu lenye alama ya kuuliza hii? nisije nikaitwa popote kuulizwa kuwa nimetoa statement yoyote, unless kwenye janga hili la Corona, hata sisi waandishi haturuhusiwi kuuliza chochote, hata ukisikia chochote kinachohatarisha usalama wa taifa letu tunyamaze tuu tukisubiria hadi hao wasemaji 4 waseme, wasiposema, tupotezee huku tunateketea?.
- Rais wa JMT
- Waziri Mkuu
- Waziri wa Afya
- Msemaji Mkuu wa Serikali
Kufuatia janga la Corona, tunahimizwa tusitangaze taarifa yoyote bila kuipokea kutoka Vyanzo rasmi vya kiserikali.
Lakini inapotokea wewe ni mwandishi wa habari makini na Mzalendo unao jua wajibu wako kama mwanahabari na wajibu wako kwa taifa lako, ukipokea habari kutoka chanzo ambacho wewe unakiamini, na ukathibitishiwa kuwa serikali inajua ila imenyamaza, kwa vile kunyamaza huko kunaweza kutusababishia majanga, hiyo kuitangaza taarifa hiyo ili serikali ichukuwe hatua stahiki ndio uzalendo wa kweli kwa taifa lako.
Mimi licha ya kuwa ni mwana habari, pia nimebahatika kufuta tongo tongo za sheria, hivyo, ili ku tie in all loose ends kunizuia nisiitwe popote kuwajibishwa kisheria, naitoa taarifa bila kutaja majina yoyote, sijasema ni Waziri gani, au waziri wa wapi, hii ili kuisaidia serikali yetu ya JMT, kutimiza wajibu wake wa kuwalinda Watanzania dhidi ya maambukizi ya Corona huku nikiheshimu haki zote za the right to privacy za wagonjwa na za watu, na ningeomba hata miongoni mwa wachangiaji ikitolea ukawa unamjua, ili kuheshimu haki za mgonjwa, nawaomba msimtaje kwa majina.
Nimepokea taarifa hii kutoka very reliable source.
... jina limehifadhiwa (Waziri wa ...) ashukiwa kuugua CORONA.
************************************************************************
Waziri wa... ambaye alikuwa safarini akitua nchini kutokea London (Uingereza [emoji636]) ambapo safari yake ilianzia Italy [emoji634] kisha kurejea wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya ... akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA.
Dr. Mkuu wa Hospitali ya ... baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya ... akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Corona, itakuwa ni aibu kwake na kumdhalilisha!.
Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika... Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA [emoji3083]
Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda , kituo Maalum cha wagonjws wa Corona, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya Italy kisha kupitia London kurejea Tanzania na homa kali!
Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya hiyo alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake.
Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali hiyo pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine.
Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Watanzaia wote!... Ameitaka serikali kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya hiyo haraka kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari!
Mwisho.
My Take.
Kwa vile Corona ni issue za kitabibu, sio lazima kila anayeugua mafua makali ni Corona, inawezeka Waziri ana homa tuu ya kawaida na mafua ya kawaida lakini sio Corona, kama madaktari wanasema sio Corona then sio Corona!.
Lakini kama ni Corona,
Natoa Wito, Only The Truth & Transparency ndio The Only Way Out Kushinda Vita Hii. Kama Waziri amepimwa na ikathibitishwa ni anaugua Corona, then his/her rights to privacy ziheshimiwe kwa kuwa upheld kwa kutokutajwa kwa jina wala wizara yake, ila asipewe any preferential treamement kwasababu yeye ni Waziri, kama mtu ameugua Corona, haijalishi yeye ni nani, msifiche waziri wetu kuugua Corona, ugonjwa wa Corona ni ugonjwa tuu hauchagui wa kumpata na sio ugonjwa wa aibu kusema tuufanye siri, unaficha nini?!. Marais wa dunia wame test positive na wametangaza, mawaziri wakuu wa dunia hadi mwana mfalme ametangaza ndio itakuwa waziri?.
Kama ni kweli kuna Waziri anaugua Corona halafu tunaficha kwasababu yeye ni Waziri, naomba kutoa angalizo la kisa cha mficha maradhi kisije..., nini huwa kinatokea ambacho Kitamuumbua. Naomba Tanzania tusifike huko!
NB. Naombeni tusianze kupiga ramli chonganishi kwa kuanza kumhisi na watu humu kutaka kumjua ni waziri gani, " umdhanie ndiye, siye!". Inawezekana ikawa ni jamaa mmoja tuu jina lake Waziri!
I wish you Saturday night njema.
Paskali
ha ha ha!!! rafiki yake enhe? ile siri ilokuwa sio siri imefichuka na kuwekwa wazi!!! Dua na sala zetu kwa muuguzi Fatma Kamusi, hakustahiki kuambukizwa ugonjwa huu kwa namna hii.
Wa uingereza bila tashwish na kujibagaza alikiri hadharan huyu wetu bila shaka kaitolea macho hiyo corona ya kibeberuYaani ni hatari kwa kuwa Waziri ameugua? Kuna Waziri Mkuu wa Uingereza naye ameugua!
Update
Wanabodi, hii sasa sio tetesi tena, leo imethibitishwa rasmi Bungeni Dodoma, kuwa ni kweli kuna Waziri aliugua Corona na akagoma kwenda kutibiwa kwenye hospitali maalum iliyotengwa na badala yake akalazimisha kutibiwa hospital ya kawaida.
Serikali ilipopata taarifa ilituma watu wake na Waziri huyo alihamishwa kikuku na kuhamishiwa eneo rasmi lililotengwa, sasa anatibiwa huko na anaendelea vizuri.
Uthibitisho huu umetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya ofisi yake, katika hotuba iliyotangazwa live, mubashara kupitia TBC.
Waziri Mkuu amevishukuru sana vyombo vya habari kwa kutangaza habari kama hizi, ambazo zimeisaidia serikali kujua na kuchukua hatua.
JF ndicho chombo pekee rasmi cha habari kwa hapa nchini kuitangaza habari hii hivyo kuiwezesha serikali kuchukua hatua stahiki.
Nami niliyewaletea taarifa hii, naomba kumshukuru sana kwa dhati yule mshirika wangu muhabarishaji kutoka Zanzibar ambaye ni binti mrembo wa Kizanzibari anayejiheshimu na mimi namheshimu sana, Asante sana mwananahabari binti mwanamke shujaa wa Kizanzibari.
Kwa heshima ya mhe. Waziri na kwa kuzingatia maadili ya kidakitari ya kitu kinachoitwa " the confidentiality clause" cha kuficha siri ya mgonjwa kati ya dakitari na mgonjwa, na kwa kutumia kipengele cha " the right to privacy" kwa sisi waandishi kutuingilia faragha za watu, Waziri Mkuu hakulitaja jina la Waziri huyo, na mimi hapa naomba nisilitaje jina la Waziri huyo na kukuomba hata wewe, hata kama unalijua jina la Waziri huyu, tusilitaje.
Information is power, hongera kwa wewe mwana jf to be the first to know, na ukiwa na taarifa yoyote kama hii ambayo italisaidia taifa, usisite kuileta humu jf.
Nawatakia siku njema.
Paskali
Update
Wanabodi, hii sasa sio tetesi tena, leo imethibitishwa rasmi Bungeni Dodoma, kuwa ni kweli kuna Waziri aliugua Corona na akagoma kwenda kutibiwa kwenye hospitali maalum iliyotengwa na badala yake akalazimisha kutibiwa hospital ya kawaida.
Serikali ilipopata taarifa ilituma watu wake na Waziri huyo alihamishwa kikuku na kuhamishiwa eneo rasmi lililotengwa, sasa anatibiwa huko na anaendelea vizuri.
Uthibitisho huu umetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya ofisi yake, katika hotuba iliyotangazwa live, mubashara kupitia TBC.
Waziri Mkuu amevishukuru sana vyombo vya habari kwa kutangaza habari kama hizi, ambazo zimeisaidia serikali kujua na kuchukua hatua.
JF ndicho chombo pekee rasmi cha habari kwa hapa nchini kuitangaza habari hii hivyo kuiwezesha serikali kuchukua hatua stahiki.
Nami niliyewaletea taarifa hii, naomba kumshukuru sana kwa dhati yule mshirika wangu muhabarishaji kutoka Zanzibar ambaye ni binti mrembo wa Kizanzibari anayejiheshimu na mimi namheshimu sana, Asante sana mwananahabari binti mwanamke shujaa wa Kizanzibari.
Kwa heshima ya mhe. Waziri na kwa kuzingatia maadili ya kidakitari ya kitu kinachoitwa " the confidentiality clause" cha kuficha siri ya mgonjwa kati ya dakitari na mgonjwa, na kwa kutumia kipengele cha " the right to privacy" kwa sisi waandishi kutuingilia faragha za watu, Waziri Mkuu hakulitaja jina la Waziri huyo, na mimi hapa naomba nisilitaje jina la Waziri huyo na kukuomba hata wewe, hata kama unalijua jina la Waziri huyu, tusilitaje.
Information is power, hongera kwa wewe mwana jf to be the first to know, na ukiwa na taarifa yoyote kama hii ambayo italisaidia taifa, usisite kuileta humu jf.
Nawatakia siku njema.
Paskali.
Jina la Paskali ni mtu aliyezaliwa siku ya Pasaka.Sasa wewe jina lako sahihi ni lipi hapo? Pascal au Paskali?
Mkuu Michael Makene, asante nimekisikia, na karibu mitaa hii....wewe ndg nilikua nakukubali Sana kwenye uchambuzi na kuusema ukweli bila kumungunya maneno lakini tokea uende kwenye kamati ya job umekua muoga balaa....simama katika ukweli itetee nchi yako washauri watawala bila kuogopa Kama watanuna hii taifa ni lakwetu sote mlipuko ukizidi tutaumia sote....waandishi nguri Kama wewe ndio wakati wenu wakupaza sauti mliponye taifa Kama mnashindwa kukemea muonapo kusua sua kwa wenye dhamana basi toeni elimu kwa jamii namna ya kujikinga na maambukizi
Sheria ya right to privacy inataka mtu ajitaje mwenyewe, na sio kutajwa na wengine. Hata kule kutajwa anatajwa Waziri tuu bila kutajwa jina lake.Kwa nini unaogopa hadi sasa kumtaja jina lake, ilhali limeshatajwa bungeni. Sema tu ni...waziri wa ... Zanzibar
Hii nimeipenda onghwise [emoji120][emoji122]. Umelifanyia utafiti jina lako. Wengine mambo haya hatuyawezi sijui ni uvivu ?!Jina la Paskali ni mtu aliyezaliwa siku ya Pasaka.
Akiwa mwanaume ni Paskali akiwa mwanamke ni Paskalia, Paskalina, Paskazia.
Kiitalina wanaandika Paschal, Kifaransa, Pasco, Kiingereza Pascal na Kiswahili ni Paskali
Lugha nyingine ni Pasqwa, Pascoe, Pascale, Pascalle, Paschal, Paskal, Pashk, Paschalis, Pascaline, Pasquale, Pascual, Pascoe, Pasco.
Jina langu ninalotumia sasa at the age of 50+ ni Paskali. At 60 nitaanguliza Mzee Paskali.
Nilipojiunga JF nilikuwa kijana nilikuwa Pasco.
Jina rasmi linavyo andikwa ni Pascal
P
Sheria ya right to privacy inataka mtu ajitaje mwenyewe, na sio kutajwa na wengine. Hata kule kutajwa anatajwa Waziri tuu bila kutajwa jina lake.
P