Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Makonda hafichi mtu, amesema yeye ana wajibu wakulinda usalama wa watu wa Dar es salaam.
Lets wait and see.
Commander In Chief imekuwaje umekimbia vita na kuonekana unakunywa kahawa mafichoni? Hii kazi ya kuongoza mapambano mbona inaonyesha kukushinda? Unapenda sifa tuu!😇😇😇
 
Wanabodi,

Naomba kuanza na Angalizo: Mamlaka pekee za kutangaza status report ya ugonjwa wa Corona kwa Tanzania ni
  1. Rais wa JMT
  2. Waziri Mkuu
  3. Waziri wa Afya
  4. Msemaji Mkuu wa Serikali
Hivi wajameni hii siyo taarifa ya update ya Corona, hili ni swali nimeuliza na alama kabisa ya kuuliza! Mimi mwenzenu kazi yangu ni kuuliza tuu maswali, na kuna swali niliwahi kuuliza, hadi nikaitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge, kuwa nimetoa statement, kumbe sikutoa statement yoyote bali nimeulizwa swali tu, hivyo bandiko hili nalo ni swali tu lenye alama ya kuuliza hii? nisije nikaitwa popote kuulizwa kuwa nimetoa statement yoyote, unless kwenye janga hili la Corona, hata sisi waandishi haturuhusiwi kuuliza chochote, hata ukisikia chochote kinachohatarisha usalama wa taifa letu tunyamaze tuu tukisubiria hadi hao wasemaji 4 waseme, wasiposema, tupotezee huku tunateketea?.

Kufuatia janga la Corona, tunahimizwa tusitangaze taarifa yoyote bila kuipokea kutoka Vyanzo rasmi vya kiserikali.

Lakini inapotokea wewe ni mwandishi wa habari makini na Mzalendo unao jua wajibu wako kama mwanahabari na wajibu wako kwa taifa lako, ukipokea habari kutoka chanzo ambacho wewe unakiamini, na ukathibitishiwa kuwa serikali inajua ila imenyamaza, kwa vile kunyamaza huko kunaweza kutusababishia majanga, hiyo kuitangaza taarifa hiyo ili serikali ichukuwe hatua stahiki ndio uzalendo wa kweli kwa taifa lako.

Mimi licha ya kuwa ni mwana habari, pia nimebahatika kufuta tongo tongo za sheria, hivyo, ili ku tie in all loose ends kunizuia nisitwe popote kuwajibishwa kisheria, naitoa taarifa bila majina, sijasema ni Waziri gani, au waziri wa wapi, hii ili kuisaidia serikali yetu ya JMT, kutimiza wajibu wake wa kuwalinda Watanzania dhidi ya maambukizi ya Corona huku nikiheshimu haki zote za the right to privacy.

Nimepokea taarifa hii kutoka very reliable source.

... jina limehifadhiwa (Waziri wa ...) ashukiwa kuugua CORONA.
************************************************************************
Waziri wa... ambaye alikuwa safarini akitua nchini kutokea London (Uingereza 🇬🇧) ambapo safari yake ilianzia Italy 🇮🇹 kisha kurejea wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya ... akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA.

Dr. Mkuu wa Hospitali ya ... baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya ... akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Corona, itakuwa ni aibu kwake na kumdhalilisha!.

Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika... Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA 🦠

Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda , kituo Maalum cha wagonjws wa Corona, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya Italy kisha kupitia London kurejea Tanzania na homa kali!

Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya hiyo alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake.

Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali hiyo pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine.

Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Watanzaia wote!... Ameitaka serikali kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya hiyo haraka kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari!
Mwisho.
My Take.
Kwa vile Corona ni issue za kitabibu, sio lazima kila anayeugua mafua makali ni Corona, inawezeka Waziri ana homa tuu ya kawaida na mafua ya kawaida lakini sio Corona, kama madaktari wanasema sio Corona then sio Corona!.
Lakini kama ni Corona,
Natoa Wito, Only The Truth & Transparency ndio The Only Way Out Kushinda Vita Hii. Kama Waziri Anaugua Corona, His/Her Rights To Privacy Be Upheld kwa kutokutajwa kwa jina wala wizara yake, ila Asipewe Any Preferential Treamement Kwasababu ni Waziri, Kama Ameugua Corona, Msifiche Waziri Wetu Kuugua Corona, Ugonjwa wa Corona sio ugonjwa wa aibu kusema tuufanye siri, Unaficha Nini?!. Marais wa dunia wame test positive na wametangaza, hadi mfalme ametangaza ndio itakuwa waziri?.

Kama ni kweli kuna Waziri anaugua Corona halfu tunaficha kwasababu yeye ni Waziri, Naomba kutoa angalizo la Kisa Cha Mficha Maradhi, nini huwa kinatokea ambacho Kitamuumbua. Naomba tusifike huko!

NB. Naombeni tusianze kupiga ramli chonganishi kumjua ni waziri gani, " umdhanie ndiye, siye!". Inawezekana ikawa ni jamaa mmoja jina lake Waziri!

I wish you Saturday night njema.

Paskali
Ahsante sana ndugu. Hapo umemaliza
 
Kifo kifo hakina huruma....tilitiliii tiliitiilii....

Alisikika mwanamuziki mmoja R.I.P akiimba na guitar lake...

Huyo ahamishwe kinguvu ugonjwa huu hauchagui hadhi sawa tu na kifo.
Walipoziandaa hizo CORONA designated hospitals walijua watakaolazwa ni maskini??
Islaaammaaabaaad....😡

Everyday is Saturday....................... 😎
 
Asante Sana Kwa taarifa. Viongozi Weng wa kiafrika ni ignorant na selfish. Ingekua North Korea huyu angewawa
Na familia yake ingepelekwa kwenye labor camps Kwa penalties na milele kutoshiriki uongozi katika nchi. Msaliti hafai ishi.
I hope si kweli Bali ni tetesi tu. Na Kama ni prof basi huyo atakua ni jalala hasa.
angetandikwa bomu kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imethibitika ana corona au haijathibitika? Huu uzi sijauelewa kabisa unataka nini?
Inaelekea akili zimeshukia tumboni. Fanya haraka tafuta sehemu tundika miguu juu kichwa kiwe chini ili akili zirudi sehemu yake, utaelewa uzi unataka nini
Vinginevyo muda si mrefu choo kitakuita ukanye,baada ya hapo hutoelewa chochote maisha mwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mayalla ni muhujumu uchumi kwanini una muhusisha waziri na kuumwa corona

Ila sipati picha ya macho ya profeseri na kuumwa haya mafua jicho lake litkuwa nyanya

Sent using Jamii Forums mobile app


Mayalla kaingia kiwoga sisi tunaweka wazi huyo ni hawa Vibaraka wa Dodoma walioko huku Zanzibar , wanaongeza tobo kwenye Jahazi ili lizame haraka pamoja na sisi maana nchi imewashinda. Tembea tembea zao huko Ulaya sasa wametuletea huo ugonjwa hapa Zanzibar . Ni Kibaraka waziri wa Nishati wa Zanzibar Salama Aboud Talib.

Na kuna tetesi kibaraka mwengine waziri wa Elimu wa Zanzibar ameonyesha mild symptoms lakini amekubali kuji isolate mapema
 
Mayalla kaingia kiwoga sisi tunaweka wazi huyo ni hawa Vibaraka wa Dodoma walioko huku Zanzibar , wanaongeza tobo kwenye Jahazi ili lizame haraka pamoja na sisi maana nchi imewashinda. Tembea tembea zao huko Ulaya sasa wametuletea huo ugonjwa hapa Zanzibar . Ni Kibaraka waziri wa Nishati wa Zanzibar Salama Aboud Talib.

Na kuna tetesi kibaraka mwengine waziri wa Elimu wa Zanzibar ameonyesha mild syptoms lakini amekubali kuji isolate mapema

Mkuu, mbona tumeambiwa mwenye dhamana ya kutangaza hayo majina ni wale wakuu watatu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni kweli kwa level yake alitakiwa kujitenga kabisa. Ila sishangai wanasiasa wana hulka sometimes ya kujifanya ni zaidi ya binaadamu wengine wakati wote tukifa tunazikwa ardhini.
Hawa viongozi wa tanzania wanaupufu fulani, ukiwauliza majina, utajibiwa kwa ukali,wewe hunijui mimi?
Akiwa mstaarabu kidogo, ataanza na neno mheshimiwa waziri...... Mh diwani....... Mh mkuu wa mkoa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chezea Coronavirus mzee baba huyo baruti Chato hana muda wa kuongoza vikao vya baraza la mawaziri lenye wagonjwa wa Corona.

Halafu kufika Chato ndio anajifanya sterling kunywa kahawa mtaani, harudi Dar akafanye zile stunts zake ubungo stand ndio tuone kweli aamini kwenye maswala ya social distancing.

Hila huko wizara ya afya watakuwa wanasema boss kweli wamepata wakati wao wanaimiza wananchi wafanye A, mwenzao bwana mkubwa anafanya B; ni shida.
 
Back
Top Bottom