Je, ni kweli kunywa maji kwa wingi kunazuia kupata maambukizi ya COVID19?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Japokuwa ni muhimu kunywa maji kwa wingi wakati unaugua ugonjwa wowote unaosababishwa na Virusi, maji hayo hayazuii wewe kupata virusi hivyo. Madai kuwa maji hayo yatazuia virusi kutoka kwenye koo kwenda kwenye mapafu, si kweli

#Coronavirus huambukizwa kwa kupitia maji maji yaliyopo kwenye mfumo wa hewa wakati mtu anapopiga chafya, anapokohoa au unaposhika sehemu yenye maji maji hayo na kujishika uso

Virusi hivi huingia kupitia macho, pua au mdomo hadi kwenye mfumo wa upumuaji ambapo husababisha madhara. Hata kama maji yangesaidia, virusi tayari vingekuwa vimesha ingia na kuleta madhara
 
Upvote 0

Hapana huu ni upotoshaji mkubwa; epuka mikusanyiko, baki nyumbani, nawa mikono kila ugusapo vitu vinavyoguswa na watu wengine. Kuweka kinga ya mwili vizuri kunywa juice ya moto ya limao na tangawizi mara kwa mara. Hii sio kinga ya corona bali inaweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mengi ya kuambukizwa.
 
Mmmmmh.... Watanzania wakipata nafuu na jambo mengi utayasikia ya waganga matapeli.
 
Ingekuwa kweli Corona ingekuwa imeisha,hii si kweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom