MWANZA
1.ni jiji la pili kuanzishwa baada ya Dar es salaam na pia ni jiji la pili kwa wingi wa watu baada ya Dar na pia ni jiji la pili kwa utajiri (GDP) baada ya DSM.
2.Jiji la Mwanza linaact kama kitovu cha kanda ya ziwa na kuwa hub kwa mikoa ya MARA,SIMIYU,GEITA,SHINYANGA,KAGERA.
3.Jiji la Mwanza limezungukwa na ukwasi wa rasilimali za kila aina kuanzia ziwa Victoria na uvuvi na migodi mikubwa mingi ya mikoa ya pemben ambayo wanufaika wake wengi na wakubwa huishi na kuwekeza zaid katika jiji la Mwanza hii hufanya Mwanza kuwa na mzunguko mkubwa saana wa pesa na pia watu wake wengi ni matajiri hili linadhihirika kwenye maeneo kama Capri point, Pasiasi n.k.
4.Mwanza kutokana na mzunguko mkubwa wa pesa limekuwa ni jiji linalotegemea zaid biashara na sekta binafsi kuliko sekta ya umma.
5.Mwanza ni kiunganishi kikuu cha Tanzania na nchi za maziwa makuu kama Kisumu kenya na Kampala Uganda.
6.Mwanza ukuaji wake ni wa uhakika sababu inajazwa na mikoa zaid ya 6 na kigezo kikuu kikiwa ni biashara na sio utawala (administration).
7.CBD ya Mwanza ni kubwa zaid kuliko majiji yote ukitoa tu DSM.
8.jiji la Mwanza linakua kwa haraka saana na limeungana hakuna space au magap ndani yake mji mzima umeungana.
DODOMA
1.Ni jiji jipya lililoanzishwa takriban miaka mitatu ilyopita likiwa na idadi ndogo ya wakaazi weng wao wakiwa ni watumishi wa umma na msingi mkubwa wa uchumi wake ukiwa unategemea uwekezaji wa miradi ya sekta ya umma.
2.Ukitoa watumishi wa umma hakuna muingiliano mkubwa saana wa watu napia hakuna biashara nyingi na kubwa na wananchi wengi wa kawaida ambao sio wafanyakazi wa umma maisha yao ni ya kawaida saana.
3.DODOMA hakuna shughuli nyingi za kiuchumi bali shughuli nyingi ni za kuitawala.
4.kutokana na msukumo mkubwa unaofanywa na serikali siku za mbeleni huenda DODOMA ikawa na miundombinu bora saana kupita Mwanza na hata majiji mengine ukitoa DAR ES SALAAM na hapa ntaitaja baadhi ya miradi hyo.
-DODOMA outer ring road 112km dual carriageway itoshe tu kusema hakuna kitu kama hiki popote pale Africa mashariki.
-DODOMA middle ring road 48km dual carriageway.
-DODOMA msalato international airport hii ni airport bora saana kwa design zake nadhani itashindana na KIA na JNIA pekee ila kwa Mwanza hapa itabid wawe wapole.
-DODOMA mtumba government city hii ni project ya aina yake kabisa ambayo pindi itakapo kamilika itabadilisha kabisa mandhari ya jiji la Dodoma.
-University of Dodoma chuo hiki kwa kweli miundombinu yake ni phenomenon ukiwa ndani ya chuo hiki unaweza kusema UDSM ukiitoa ile library mpya ni just highschool tu kimajengo ([emoji1787][emoji1787][emoji1787] kidding)
-Benjamin mkapa hospital kuna uwekezaji mkubwa saana unaofanya ndani hospital hii katika kuiboresha wodi nying zimeanzishwa kama za figo na nyingne nying zipo njian kuanzishwa kama wodi ya saratani.
Hii itoshe tu kama sample ila ipo mingine ming tu.
5.DODOMA wameanza vizuri kwa kuwa na master plan yakisasa, kuongoza kwa mapato ktk majiji isipokuwa DSM, pamoja na kuwa na timu katika ligi kuu na kuyapiku majiji ya Arusha na Mwanza ambayo hayana timu katika ligi kuu.
MWISHO
-Mwanza kwa hivi sasa iko mbaal saana kuilinganisha na DODOMA, CBD ya DODOMA ni kama tu kata ya nyakato Mwanza ambayo ipo nje ya mji.
Mwanza ni mji unaojengwa na watu wenyewe kibiashara wakat DODOMA ni mji unaojengwa na serikali kiutawala,
Mwanza wananchi wanapesa kuliko wafanyakazi wa umma wakati Dodoma wenye pesa weng ni wafanyakazi wa umma.
In a long run maybe 10yrs to come DODOMA inaweza kucompete na Mwanza ila sio sasa.