Je, ni kweli kuwa Serikali yetu imekosa kabisa ubunifu wa kuzuia ufujaji wa pesa za umma katika miradi ya kuboresha maisha ya watu maskini?

Kwa kweli sintashangaa kabisa kwa sababu kila leo ni bora kuliko jana
Watz hawana tabia ya kuhama nchi yaani anaona ataanzaje maisha mapya
Watakaa hapo hapo bila mabadiliko
Jembe la mkono hesabu miaka 50 mingine
Yaani unaona kabisa kila awamu ikiingia ina mpango wake. Awamu ikiisha mipango ya awamu iliyopita inafutiliwa mbali. Serikali haina malengo ya muda mrefu. Viongozi wako tayari kuingia mikataba itakayowapa faida papo kwa hapo. Bila kujali athari ya miaka ijayo kwa nchi kiujumla.
 
Hakuna Rais wa kupambana na RUSHWA hapa. Ni nani mwenye akili Sawa Sawa anaweza kumuelewa hata dhamira yake. Yupo yupo tu Bora liende. Hasara mno kwa nchi kuwa naye huyu
 
Wanatuibia halafu wanakimbilia kwenye kutunza amani shuwani
 
Huyo bib kama alijua hawezi kuingoza si angekaa tu pembeni jamani. Hi ni aibu kuwa na riaisi wa nchi asiyejua abc
 
Mkuu unakosea sana kuamini kwamba tuna serikali au viongozi wenye nia ya thati kuleta maendeleo..!! Ni nchi pekee dunian ambayo wananchi hawaangaiki na serilali yao, na serikali nayo haihangaiki na wananchi wake! Uliona wapi report za CAG zinatoka na madudu kila mwaka na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa!! Serikali, bunge, na wananchi wote wamekaa kimya as if hamna kilichotokea! Kimsingi tuna viongozi wezi na wala rushwa wakubwa! Ni vigumu sana kwa nchi ya namna hii kupiga hatua kwenye maendeleo ya ukweli, hasa pale viongozi wanapofikiri kuwa maendeleo ni "hisani" na sio jambo la lazima!

Mbaya zaidi wanaapa kwa vitabu vitakatifu, ila hakuna hata mmoja anayekumbuka kile kiapo alichoapa. Kuna wabunge na mawaziri unaweza kusema ni "cartoons" (Im sorry to say this). Ukiangalia upuuzi wanaofanya na hoja walizonazo ndo utajua hawana vision yoyote kwa siku za usoni. We uliona wapi dunia hii mtu anapewa wadhifa kwa sababu ya kusifia mtu mwingine badala ya merit? Haijalishi kwamba ana uwezo wa kufanya kazi, ila kwa kuwa ana uwezo wa kusifu tu, anapewa wadhifa (shame on us kwa kweli). Imefika mahali vijana wanaitwa "chawa", and they feel it's OK. Kisa cha kuitwa chawa ni uwezo wa kusifia hata ujinga!! Sasa chawa unategemea alete maendeleo kwa wananchi? Chawa huwa ananyonya damu tu, hajali kuwa utakufa au utapona.

We Endelea kufikiria kuhusu katiba itakayowapa wananchi mamlaka. Kwa sasa wananchi wanaonekana km manyani tu na ndio maana wengine wanasema "kama unaona tozo ni ngumu, hamia Burundi". Kama unamheshimu aliyekupa kura, na unaamini bila yeye usingefika hapo, unapata wapi ujasiri wa kumkejeli namna hiyo????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…