Tetesi: Je, ni kweli kuwa siku hizi ukifanya miamala mikubwa benki unafuatiliwa hata akaunti kushikiliwa?

aiseeh Nasikia kuna mama mmoja kariakoo kanunua nyumba tabata, wamemchunguza hadi dukani kwake anavyouza na kuingiza wakamuomba risiti za miaka 5 iliyopita tangu alipoanza biashara! chanzo ni vile kanunua nyumba

Hatari sana. Kwa wafanya biashara muhimu sana kutunza kumbukumbu. Pia naona fursa kwa wahasibu kuwafanyia mahesabu na kuwawekea kumbukumbu zao wafanya biashara wadogo wadogo ili kuweka mahusabu yao vizuri. Itawaokoa na mambo mengi pia kuwasaidia kuhakikisha wanalipa zile kodi stahiki na hawaingii kwenye migogoro na TRA.
 
Kuna 700mil za "ganji" ya kusepesha gold huko Mwanza hazijulikani zilipo,,
Tuvumiliane tuuu hadi zitakapo patikana,,
 
HIVI KAMA MTU KAVUNJA KIBUBU CHAKE HILO LIPOJE?

Bado watataka kujua shughuli zako kuu za kukuingizia kipato ili waridhike kwamba unuwezo wa kuhifadhi pesa kwenye kibubu ya hicho kiwango. Lakini hapo wajuvi watakuja kutupa muongozo sheria inasemaje kwa hayo mazingira.
 
sasa kama umevunja kibubu unawaambiaje?

Sasa mkuu si unawaambia umevunja kibubu kwani useme vipi tena wakati umevunja kibubu?
Watajiridhisha kwa kukufanyia tathmini ya kipato chako kuona kama kinaendana na maelezo yako.
 
KWA MFANO PESA ZA UDALALI INAKUWAJE? Mfano mtu kadalalia cha juu 50mil unaanzaje kupata documents?
 
KWA MFANO PESA ZA UDALALI INAKUWAJE? Mfano mtu kadalalia cha juu 50mil unaanzaje kupata documents?

Udalali mbona wenzako wana ofisi zao na wanalipa kodi? Swali la msingi ilikua benki kuhoji unapofanya miamala mikubwa, nimeshakwambia bila kujali pesa umeipata wapi utaulizwa, hakuna haja ya kuogopa wala kuwa na mashaka kama vyanzo vyako vya mapato ni halali alimradi uwe na nyaraka.

Huyo mfanyabiashara anaenunua nyumba yenye 50M ya udalali mara nyingi atakua anajielewa kuhakikisha mambo ya nyaraka yamekaa sawa. Vinginevyo na yeye pesa yake iwe ya mashaka.
 
Sasa mkuu si unawaambia umevunja kibubu kwani useme vipi tena wakati umevunja kibubu?
Watajiridhisha kwa kukufanyia tathmini ya kipato chako kuona kama kinaendana na maelezo yako.
fundi au muosha magari unaanzaje kumfanyia tathimini?
 
DALALI OFISI YAKE CHINI YA MWEMBE; akilipwa apeleke documents gani?
Au muosha magari aliyechonga kibubu akikipasua apeleke documents gani?
 
Hiyo system ya kufuatiliwa sana imeanza sasahivi japo zamani ilikuwepo ila sio sana.

Sahizi watakaokuwa wanaweka Pesa ni wale wa mishahara na vilaki laki ndio watabaki kutumia bank ila wafanyabiashara wa mamilioni itakuwa ni "hand to hand'
 
Acha kudanganya watu hakuna kitu km hichp 5m?? 15??? tangia lini benk ikuhoji hiyo ni pesa ndogo sn

Sent using Jamii Forums mobile app
Unavyoongea kwa kujiamini.
Nina mashaka iwapo unafanya miamala Mingi Benki Miaka miwili au mitatu hii.
Ni utaratibu wa kawaida sana mbona hata 3Mil.unaulizwa aamue kupuuza utaratibu tu teller husika.
 
Hiyo system ya kufuatiliwa sana imeanza sasahivi japo zamani ilikuwepo ila sio sana.

Sahizi watakaokuwa wanaweka Pesa ni wale wa mishahara na vilaki laki ndio watabaki kutumia bank ila wafanyabiashara wa mamilioni itakuwa ni "hand to hand'
Exactly. Pamoja na kutumia external wallets kama bitcoin, paypal etc

Kuweka pesa ndefu bank za Tanzania ni very risky business

Sent using Sukhoi Su-57
 
acheni kudanganya umma. hakuna wa kukuuliza , nimeuza toyota harrier new model this january jamaa kaingia CRBD internet banking kahamisha mzigo wa kutosha kwa accnt yangu (more than 19M) , hakuna wa kuniuliza wala jamaa hajaulizwahadi leo. ...hzo mambo za kuulizana pesa umetolea wapi ni kama unafanya transaction counter ama vp ?

All is Well
 
Imeanza lini hii

Noma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…