Tetesi: Je, ni kweli kuwa siku hizi ukifanya miamala mikubwa benki unafuatiliwa hata akaunti kushikiliwa?

Acha kudanganya watu hakuna kitu km hichp 5m?? 15??? tangia lini benk ikuhoji hiyo ni pesa ndogo sn

Sent using Jamii Forums mobile app
Pesa ndogo kwako au kwa nani? Mwaka 2014 nilikuwa natuma 1900USD (3.3mil wkt huo) nje kununua bidhaa, kwenye fomu nikaruka kipengele cha kueleza ni pesa ya nini, ile fomu ilirudishwa nijaze hicho kipengele ndio pesa itumwe. Ilikuwa pale CRDB Azikiwe. Hiyo 2014, leo hii 2019....
 
Kwa hali ya usalama wa ukanda kwa sasa, njia moja wapo ya kudhibiti uhalifu mkubwa ni pamoja na kufuatilia miamala. Kwa mfano, ikiwa wewe unakawaida ya kufanya miamala ya 10,000 mpaka Milioni 1, halafu ghafla ukafanya muamala wa milioni 30, lazima kama benki watoe ripoti. Hii hutokea hasa kama, umewekewa hela kwenye akaunti na mtu au taasisi ambayo haitambuliki vizuri, haina uhusiano na shughuli zako au hata haikutolea maelezo ya kujitosheleza kwenye sababu za muamala huo.

Laiti vyombo vyetu vya usalama vingejikita kwenye elimu kwa raia ili kupunguza taarifa zisizo rasmi kuenea na kupotosha.
 
Nisiwe mwongo sijawahi kuhojiwa wala kufuatiliwa, labda kufuariliwa iwe kimyakimya. Lakini ni kweli kua wanauliza na kufuatilia hata kama ni nyumba umauza unatakiwa uende tra ukalipie kodi
 
Nilivyoelewa hajakataa hicho kipengele, yeye anamaanisha pesa za kuweka na kutoa.
 
Mwaka Juzi nilienda kufungua account Bank flani hapa Dar es salaam, na at the same time nikaweka 8 millions Cash....

Sikuulizwa hata kuwa pesa nimetoa wapi..!

Nadhani kuna kiwango flani ukiweka Bank au kupokea ndo unaweza kuulizwa, may be kuanzia 30+ millions......
 
Acha kudanganya watu wewe Kama milioni 20 mtu lazima ajieleze basi bank itabaki na kazi ya kusikiliza Maelezo ya watu kuanzia asuhuhi hadi jioni maaana watu wa anaotoa 20m na kuendelea Kwa Siku ni zaidi ya watu elfu moja Kwa Siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kudanganya watu hakuna kitu km hichp 5m?? 15??? tangia lini benk ikuhoji hiyo ni pesa ndogo sn

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaoji mkuu, mimi niliwahi kuhojiwa na Teller wa NBC pale Samora kisha akaona anipeleke kwa meneja wa benki kutoa maelezo hiyo pesa nimeitoa wapi.
Harakati za kutafuta mafanikio nikiwa mdogo ziliniponza, mwisho wakaniomba radhi kwa usumbufu mana walijua nimeiba nyumbani eti!?
 
Hivi Kama hilo ni la kweli basi bank itabaki Kwa kusikiliza Maelezo ya watu badala ya Huduma maaana huyo anaeweka au kutoa anaenda moja Kwa moja dirishani maaana yake foleeeni yooote ikiwa inaweka na kutoa above 5m wote watakaa kujieleza sio kweli haakuna kitu Kama hicho bhana ,hilo swala ni gumu na unapotaja milioni kumi na tano tambua kuwa hiyo hela ni ndogo sana yani ni pesa ndogo sana hiyo na watu wanaweka hela na kutoa kila Siku tena Wengi Sana na zaid ya hizo uzisemazo, Sema kuna mtu anaweza akaenda bank kulingana na mazingira Fulani Fulani akahojiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hujawahi kutana na hiyo kadhia ni bora ukabaki kimya mana kuna watu walishahojiwa na mimi ni mmojawapo.
 
Hata milioni 30 ni ndogo brooo, hata mia ni ndogo Sema inategemea wewe unaweka milioni mia kwenye account yako Wakati hiyo account yako haijawahi kupokea hata milioni moja hapo waweza kutoa Maelezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikuongopea napata faida gani?
Mimi nimenunua kitu kwa mtu kwa milioni 7.7 tukakubaliana kwa sababi za usalama wake na wangu nimuingizie bank 5M na 2.7 niende nayo cash serikali za mitaa.

Huyo ltu nahisi hakuwahi kuweka hata milioni 1 kwenye akaunti yake. Bank wakaniuliza mbona pesa nyingi unamuingizia za kazi gani?

Kubisha isiwe kama dini yako. Bado kunaifano mingi tu, kamapuni ninayofanyia kazi tuna kitu tunailipa kampuni flani ya huko Dubai dola kadhaa wastani wa Tshs milioni 4 - 5 kila mwaka. Kila mara bank yetu hapa bongo na ya jamaa huko Dubai wanataka vielelezo ni pesa ya nini?
 
Branch chache sana zinazofikisha robo ya idadi hiyo ya watu wanaotoa 20m na kuendelea.
Hii inaonesha wewe haufanyi kazi bank na hauwezi kukadiria idadi ya watu.

Kwanza watoa pesa nyingi kama hizo bank nyingi huchukulia sehemu maalum sio zile teller za watu wote. Huko kwenye hivyo vyumba hakuna goleni tena nyingi kuna makochi(sofa) na vinjwaji baridi ka soda, maji, chai na kahawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…