Je, ni Kweli kuwa YESHUA, Hana baba wala mama?

Je, ni Kweli kuwa YESHUA, Hana baba wala mama?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, shalom!!

Nimesoma kitabu kimoja kinaenda Kwa Jina la (Waebrania 7:3), kwamba Kuna mtu anaitwa MELKIZEDEKI, Ambaye amefananishwa na YESHUA / YESU/JESUS,Kwa sifa zake, kwamba Hana baba wala mama, Wala Hana mwanzo au mwisho wa siku zake, ni WA milele🤔

Tujadiliane hapa kiundani, Hawa wasemao Maria ni mama wa Mungu, wametoa wapi maneno haya?

Na wanaenda mbali kumuomba Maria awaombee kana kwamba Maria ana ushirika na Mungu katika maamuzi!!

Karibuni, mihemko tuweke pembeni🙏
 
Ukiona hauyaelewi yaliyomo katika Maandiko. Ujue hayakuhusu!
Maandiko yamedai tuyachunguze!!

Pia yupo Mungu Roho mtakatifu kutufunulia yaliyofichwa tusoyaelewa.
 
Bila shaka inahitaji akili kubwa kuyaelewa maandiko matakatifu ya Mungu.

Nadhani kama lengo lako ni kujua kwa nini watu humnena Maria kama mama wa Mungu wakati Mungu hana mama wala baba!

Kama hivyo ndivyo, nikuulize, Je, waamini kama Yesu ni Mungu? Naomba tuanzie hapo!
 
Ndio,

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake.

Na Mungu huyo mmoja, hana baba wala mama, Wala Hana mwanzo Wala mwisho.
 
Back
Top Bottom