tz2015
JF-Expert Member
- Jun 23, 2014
- 982
- 447
Habari zenu wanajamvi wote katika jukwaa hili.
Ni muda mrefu nimekuwa nikijiuliza kuhusiana na uhuru wa mhimili huu unaoitwa mahakama bila kupata ufumbuzi.
Swali langu linakuja pale ninapokuta mihimili mingine kama vile bunge, na serikali wanachagua viongozi wao wenyewe, mfano, wabunge ndio wanaomchagua spika wa bunge kwa utaratibu waliojiwekea na wanashiriki kugombea na kupiga kura.
Serikali nayo tunaamini wananchi ndio wadau wakuu wa serikali au kwa maneno mengine ndio waajiri wa viongozi wa umma,na wanashiriki kuiweka serikali madarakani.
Sasa najiuliza kwa upande wa mahakama ni nani kiongozi mkuu wa mahakama? kama ni jaji mkuu,mbona anateuliwa na rais na kwa mawazo yangu ni rahisi huyu mteule wa rais kuendeshwa na aliyemteua na hivyo kuufanya mhimili huu usiwe huru tena bali kuwa taasisi ya serikali.
Nimeleta kwenu wanajamvi kwa anayejua aniondolee ujinga huu.
Naomba kuwasilisha kwa majadilianao.