Imekuwa ikidaiwa mara kwa mara kwamba marubani wa ndege hawaruhusiwi kula chakula cha aina moja wanapokuwa safarini, hasa rubani mkuu na msaidizi wake. Suala hili limekuwa likiendelea kwe kampuni mbalimbali za usafiri wa anga.
- Tunachokijua
- Kila ndege ya kibiashara huongozwa na marubani wawili waliohitimu kikamilifu, ambao ni rubani mkuu (Captain) na msaidizi wake.
Marubani hawa wote wawili wana ujuzi na mafunzo sawa ya kuendesha, kuongoza, na kutua na ndege peke yao ikiwa mmoja wao atapata dharura au dharura yoyote ya kiusalama itajitokeza angani kulingana na muundo wa usalama wa anga.
Ili kuhakikisha usalama wa abiria na mali, marubani wanatakiwa kuwa na afya thabiti, utulivu wa akili, na umakini wa hali ya juu wakati wote wa safari, bila kuathiriwa na changamoto zozote za kiafya zinazoweza kuzuilika.
Madai
Kuna madai ya muda mrefu kwamba marubani wawili wanaoendesha ndege moja hawaruhusiwi kabisa kula chakula cha aina moja, kutoka chanzo kimoja, au kwa wakati mmoja wanapokuwa kazini safarini.
Uhalisia wa madai hayo
Madai haya ni ya kweli kabisa na yanawakilisha moja ya taratibu kali kabisa za usalama zinazofuatwa na mashirika mengi ya ndege duniani.
Ingawa utaratibu huu si sheria rasmi ya kimataifa kutoka mamlaka za usafiri wa anga kama FAA au ICAO, mashirika mengi yameifanya kuwa sera ya ndani ya lazima ili kuzuia hatari ya marubani wote wawili kupata sumu ya chakula (food poisoning) kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa utaratibu huu, ikiwa chakula cha aina moja kimechafuliwa au kina bakteria, na kikamsababishia rubani mmoja maumivu makali ya tumbo au kupoteza fahamu, rubani wa pili aliyekula chakula tofauti atabaki salama na mwenye afya njema ili kuendelea kuongoza ndege na kuitua salama kwenye uwanja wa karibu.