Uchaguzi 2020 Je, ni kweli mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM anakubalika kama mitandao inavyotuaminisha?

Uchaguzi 2020 Je, ni kweli mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM anakubalika kama mitandao inavyotuaminisha?

Sewa Sewa

Member
Joined
Aug 21, 2020
Posts
37
Reaction score
535
Habari zenu Wana wa JamiiForums,

Natanguliza kusema mimi si mwanasiasa, siijui siasa wala itikadi yeyote. Kwanza toka nizaliwe sijawahi kupiga hata kura ndio labda mwaka huu kwa mara ya Kwanza nitachagua viongozi.

Ila Nikiwa Kama kijana wa kileo na mwenye uelewa kidogo wa Mambo, kuna mambo ambayo nashindwa kujua ukweli wake. Mambo hayo Ni Kama ifuatavyo

1.Je, mgombea wa chama Cha mapinduzi anakubalika kwa kiasi gani? Mbona naona wasanii waigizaji karibia wote wakimpigia kampeni?? At mnapiga kampeni kutoka moyoni au Kuna unafiki /kujipendekeza/kutafuta nyazifa/Au Kuna malipo ndani yake??

2. Kila mtu mwenye cheo/mfanyabiashara na mtu maarufu anaonekana kutoa sapoti upande wa CCM, hizo sapoti nizionavyo kwenye mitandao si za uoga wa kwenda kinyume na dola?? Au kweli yanatoka moyoni??

Wanajamii forum naomba mtuambie hali ya huko mtaani, ukweli ukoje. Je mgombea wa CCM anaungwa mkono kwa kiasi gani??. Yani Ile ya kweli ambayo sio unafiki, Ile mkikaa wawili watatu ama kijiweni Hali ikoje?

Weka siasa kando andika kile unachokiona huko kwa majumba yenu na majirani zenu.
 
Anakubalika ila wafanyakazi wa serikali wengi ni wanyonge sana na hofu juu.
 
Anakubalika sana, tena himu kitandaoni hutapata picha halisi kwa sababu sehemu ya watanzania wanaotumia hii mitandao ni ndogo tu. Ukweli halisi uchunguze kwa watu wasiotumia hii miatandao ambao ndio wengi. Kifupi anakubalika sana
 
Lengo la uzi wako halitafanikiwa. Wewe ulitaka jibu neutral ila hapa utajibiwa kivyama, kila mtu akivutia kwenye chama chake
 
Mkuu watanzania wana akili!

Hawawezi kumchagua mtu ili awe anaongoza nchi kwa mwongozo wa Ansterdam.

Magu tano tena.
 
Anakubalika sana, tena himu kitandaoni hutapata picha halisi kwa sababu sehemu ya watanzania wanaotumia hii mitandao ni ndogo tu. Ukweli halisi uchunguze kwa watu wasiotumia hii miatandao ambao ndio wengi. Kifupi anakubalika sana
Ww anakubalika kinafki watu wameficha makucha
 
Huoni wapinzani wake wanavyoweweseka..?

Kama hakubaliki si wangejikalia kimya wachukue nchi.
 
Hakubaliki,Tabia za watz Kama za wajumbe wa ccm, waosema wanamkubali wanafiki, tarehe 28 watamtosa
 
Sasa asipokubalika Magufuli nani atakubalika mwingine
 
Mkuu rekodi ya Magufuli inambeba.

Yaani Gwajima tu anawatoa jasho mpaka mkaona umuhimu wa kufungua kampeni zenu kawe.

Huku mtaani ni kipigo tu mtapata endeleeni kujipa matumaini na kujiliwaza hapa mitandaoni.
 
Mtaani kwetu kwa kweli watu wengi wanasema kwa vyovyote vile magufuli ataipita, ni wengi kama sio wote wanakiri hivyo
 
Anakubalika sana, tena himu kitandaoni hutapata picha halisi kwa sababu sehemu ya watanzania wanaotumia hii mitandao ni ndogo tu. Ukweli halisi uchunguze kwa watu wasiotumia hii miatandao ambao ndio wengi. Kifupi anakubalika sana
Boss hawa. ambao Hawana hata laini.za simu na moster of them zile K.K.K 3 zimewapita lushoto,wanaweza kukupa taswila ya kukubalika au kutokubalika kwa JPM?.. are you serious? upo kijiji gani?

Wakipewa t shirt na kofia.wakala na wali basii wataimba na kujipaka chokaa BAADA ya hapo wanaendelea na mlo mmoja wa manati through out,,,. Uliza watu conscious
 
Back
Top Bottom