POTOSHI Je, ni kweli Michelle Obama ni mjamzito?

POTOSHI Je, ni kweli Michelle Obama ni mjamzito?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu au mimi naona vibaya? Hii picha ina ukweli kiasi gani?

MICHELLE OBAMA.jpg
 
Tunachokijua
Michelle Obama ni wakili na mwandishi, ambaye pia ni mke wa aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii hususan X, imesambaa picha ya mke wa Obama akionekana na kuwa na tumbo kubwa kuliko kawaida na hivyo kuibua mjadala mkubwa miongoni mwa watu huku wengine wakihoji kuwa ni mjamzito. Tazama hapa, hapa.

Ufuatiliaji umefanyika na kubaini kuwa picha hiyo imehaririwa kwa kumuongezea tumbo, Michelle kuliko kawaida na hivyo kupotosha uhalisia.

Picha halisi ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Aprili 2025, ambapo Michelle alionekana huko Los Angeles, Marekani ikiwa kwenye wakati ambao kulikuwa na uvumi uliokuwa ukisambaa kuwa wawili hao hawapo pamoja tena.

Tovuti ya Hola ilieleza kuwa Michelle ameonekana akiwa na pete yake ya uchumba pamoja na ndoa kufuatia uvumi wa kuvunjika kwa ndoa yao.
Back
Top Bottom