Je, ni kweli Moshi na Arusha ndo inaongoza kwa kuwa na mafundi rangi wazuri wa magari?

Habari wadau,

Ninahitaji Fundi rangi mzuri, nimefanya research kati ya watu 8 katika 10 wanasema nipeleke gari Moshi au Arusha sababu wanajua vizuri kupiga rangi.

Je, ni kweli wanapatikana huko tu?
Wewe ungeuliza tu ni garage gani Arusha au moshi naweza kupaka rangi gari?
Ukweli ni kuwa unaweza kutengenezewa gari lolote likatoka kama vile ndio limetoka japani/ulaya ILA na bei zake zimechangamka
hivyo kama ni gari la kawaida, huna haja ya kupeleka huko kwani bei itakuwa juu; ila kama ni gari la kisasa la bei ya juu songa mbele; ulizia Garage tu
 
Moshi na Arusha kumebahatika kuwa na ufundi mkubwa wa magari na kampuni kubwa za kukata Cruiser zipo huko kwa mfano Moshi kuna Rajinder na Arusha kuna Hans hao jamaa wamekuwa na mafundi kibao wa kanda hiyo na kama unavyojua jamaa walitrain mafundi kufanya kazi kidunia ya sasa na ndo sababu kubwa mafundi wa mtaani wengi unakuta walipita kweny hiz kampuni kubwa au wamefundishwa na jamaa walopita huko. hii ndo sababu kuna mafundi watundu sana kaskazini sio tu kweny rangi ila hata kuchonga body na upande wa ufundi. kama bado hujapata fundi nijuze nikupe mpare flani yupo arusha huyu anakufata ulipo.. na kazi zake ni kiwango anachukuliwaga hadi nchi jirani.
 
Dar inabaki kuwa juu
 
Hivi kweli Cfao wanakuwa na mafundi bora sana? Maana kuna mmoja namfahamu na mwingine keshastaafu huko, lakini kuna gari uwa wanalikimbia.
CFAO wana mafundi wazuri katika level. Nakumbuka zamani sana nilisha enda pale kufanya kama mafunzo flani ya ufundi kutumia cheti changu. Wale tunao ingia na mavyeti makubwa wengi wetu ni vimeo ila pia wenye mavyeti makubwa ukiwakuta deep wapo deep kweli na wengi walipitia. Ila pia pale kuna katabia ka ku specialize maeneo flani, ukimpeleke nje ya eneo lake anakimbia
 
Samahani Naomba mawasiliano yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…