barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Asante kwa elimu Dr., mimi nina swali, je ambaye hutoa maamuzi kuwa nyonga ni ndogo hivyo ufanyike operation ni daktari au muuguzi?? Samahani, ila sinaga imani sana na wauguzi ktk baadhi ya maamuzi yao!!Jibu la swali lako ni HAPANA.
Bali, inategemea nini hasa kilisababisha "oparesheni" katika huo uzao wa kwanza? Kama ni sababu ambayo ni permanent na haibadiliki, basi ndio hataweza tena kujifungua njia ya kawaida (mfano: njia ya uzazi "nyonga" ndogo isiyoweza kupitisha mtoto). Kwa hiyo basi, kama uzazi wa kwanza ulijifungua kwa mnjia ya oparesheni, na sababu ilikuwa ni ile ambayo sio ya permanent mfano kondo kutangulia (placenta previa), uzazi wa pili unaweza kujaribu kujifungua kwa kawaida (trial of scar). Lakini, hii inabidi ifanyike chini ya uangalizi, kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya wamejiandaa kufanya oparasheni muda wowote ule mambo yakienda vibaya.
Baadi ya sababu ambazo zinaweza kusababisha ushindwe kujifungua njia ya kawaida na kuhitaji "oparesheni" ni kama ifuatavyo:
-Nyonga nyembamba isiyoweza kupitisha mtoto
-Kama una ugonjwa mwingine wa muda mrefu ambao utaleta shida wakati wa kujifungua kama ugonjwa wa moyo,
-Mtoto kutanguliza miguu/matako
-Kondo kutangulia (placenta previa)
-Mtoto mkubwa kupita kiasi (big baby)
-Mimba ya mapacha wawili/watatu/wanne
-mtoto kulala vibaya (transverse/oblique lie)
-Uchungu kwenda taratibu sana au kushindwa kuprogress
-Mtoto kuchoka (fetal distress).
Ni muhimu kuelewa kuwa, sababu zote hizo hapo juu (isipokuwa ya kwanza), ni sababu ambazo ni relative; kumaanisha kwamba si lazima mfano mama akiwa na mimba ya mapacha basi ajifungue kwa oparesheni, uamuzi utategemea mambo mengi ikiwa ni pamoja na hali ya mama,etc etc.
Abuu Ibrah
Na je ni kweli kuwa nyonga kuwa ndogo yawezekana kuwa mtoto labda alikuwa mkubwa zaidi ya njia ya kutokea?? Kuna uwezekano raundi ya pili akawa mtoto ana saizi ndogo??
Nilikuwa nahitaji hii elimu, nimewahi uliza humu ila sikupewa maelezo ya kina hivyo niliingia mtandaoni na kujipatia election mu kidogo, hivyo kwa kuwa Dr. Upo naomba elimu ya ziada!
Nimeelimika pia kutokana na elimu uliotoa hapo juu, asante!!