Je, ni kweli mtu akijifungua kwa operation uzao wa kwanza hawezi tena kujifungua kawaida?

Jibu la swali lako ni HAPANA.
Bali, inategemea nini hasa kilisababisha "oparesheni" katika huo uzao wa kwanza? Kama ni sababu ambayo ni permanent na haibadiliki, basi ndio hataweza tena kujifungua njia ya kawaida (mfano: njia ya uzazi "nyonga" ndogo isiyoweza kupitisha mtoto). Kwa hiyo basi, kama uzazi wa kwanza ulijifungua kwa mnjia ya oparesheni, na sababu ilikuwa ni ile ambayo sio ya permanent mfano kondo kutangulia (placenta previa), uzazi wa pili unaweza kujaribu kujifungua kwa kawaida (trial of scar). Lakini, hii inabidi ifanyike chini ya uangalizi, kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya wamejiandaa kufanya oparasheni muda wowote ule mambo yakienda vibaya.
Baadi ya sababu ambazo zinaweza kusababisha ushindwe kujifungua njia ya kawaida na kuhitaji "oparesheni" ni kama ifuatavyo:
-Nyonga nyembamba isiyoweza kupitisha mtoto
-Kama una ugonjwa mwingine wa muda mrefu ambao utaleta shida wakati wa kujifungua kama ugonjwa wa moyo,
-Mtoto kutanguliza miguu/matako
-Kondo kutangulia (placenta previa)
-Mtoto mkubwa kupita kiasi (big baby)
-Mimba ya mapacha wawili/watatu/wanne
-mtoto kulala vibaya (transverse/oblique lie)
-Uchungu kwenda taratibu sana au kushindwa kuprogress
-Mtoto kuchoka (fetal distress).
Ni muhimu kuelewa kuwa, sababu zote hizo hapo juu (isipokuwa ya kwanza), ni sababu ambazo ni relative; kumaanisha kwamba si lazima mfano mama akiwa na mimba ya mapacha basi ajifungue kwa oparesheni, uamuzi utategemea mambo mengi ikiwa ni pamoja na hali ya mama,etc etc.
Abuu Ibrah
Asante kwa elimu Dr., mimi nina swali, je ambaye hutoa maamuzi kuwa nyonga ni ndogo hivyo ufanyike operation ni daktari au muuguzi?? Samahani, ila sinaga imani sana na wauguzi ktk baadhi ya maamuzi yao!!
Na je ni kweli kuwa nyonga kuwa ndogo yawezekana kuwa mtoto labda alikuwa mkubwa zaidi ya njia ya kutokea?? Kuna uwezekano raundi ya pili akawa mtoto ana saizi ndogo??
Nilikuwa nahitaji hii elimu, nimewahi uliza humu ila sikupewa maelezo ya kina hivyo niliingia mtandaoni na kujipatia election mu kidogo, hivyo kwa kuwa Dr. Upo naomba elimu ya ziada!
Nimeelimika pia kutokana na elimu uliotoa hapo juu, asante!!
 
Sio kweli!

Nami nimewahi fungua uzi humu kuuliza hii. Na pia nimeuliza baadhi ya madaktari na pia kusoma baadhi ya articles ktk mtandao.
Sababu ya kuzaa kwa operation yaweza kuwa ni sababu zinazosababishwa na mzazi yaani mama au sababu zinazosababishwa na mtoto, mfano mtoto kakaa vibaya, au mtoto kuwa mkubwa kuliko njia ya kupita. Kama ni hatari kwa afya ya mmojawapo, basi operationa ni njia sahihi!

Pia inasemekana ili uwe na chansi za kujifungua tena kwa njia ya kawaida ni lazima ule mpasuo wa awali uwe umepona kabisa la sivyo unaweza chanika!! Hivyo hakikisha kati ya kujifungua mtoto na mtoto kunakuwa na nafasi ya kutosha kwa mshono kupona kabisa, kwa wanawake walio chini ya thirties, mishono hupona haraka kuliko wanawake wazima zaidi yaani thirties na kuendelea. Hivyo wanawake wa below thirties na hasa below 27 wana chansi kubwa ya kuja kuzaa kwa kawaida kama uzazi wa kwanza ulikuwa ni wa operation na wanataka kuzaa kwa VAginal Birth After Caesarian ( VBAS).

Pia wanawake wengi wana condition inaitwa CEPHALOPELVIC DISPROPOTION yaani nyonga ndogo, hii haina dawa, kama nyonga ni ndogo itabidi tu afanyiwe operation ila sababu kubwa ya kuwa na nyonga ndogo ni mtoto kuwa mkubwa, hamna kitu cha kama nyonga ndogo, ishu ni mtoto kuwa mkubwa zaidi ya njia ya kupita.
Ebu google VBAC (Vaginal Birth After Caesarian) utapata elimu ya kutosha!

Ila jibu la Swali lako ni SIO KWELI ila kutokana na baadhi ya conditions yaweza ikawa hivyo, yaani itabidi uzae kwa operations mimba zinazofuata kutokana na mimba ya kwanza kuwa ya operation!!

Kawaida mshono hupona kabisa baada ya muda gani, maana mi mke wangu kabeba hii nyingine baada ya kupita mwaka na miezi 6 tangu apasuliwe, msaada kwa tena tafadhali.
 
Asante kwa elimu Dr., mimi nina swali, je ambaye hutoa maamuzi kuwa nyonga ni ndogo hivyo ufanyike operation ni daktari au muuguzi?? Samahani, ila sinaga imani sana na wauguzi ktk baadhi ya maamuzi yao!!
Na je ni kweli kuwa nyonga kuwa ndogo yawezekana kuwa mtoto labda alikuwa mkubwa zaidi ya njia ya kutokea?? Kuna uwezekano raundi ya pili akawa mtoto ana saizi ndogo??
Nilikuwa nahitaji hii elimu, nimewahi uliza humu ila sikupewa maelezo ya kina hivyo niliingia mtandaoni na kujipatia election mu kidogo, hivyo kwa kuwa Dr. Upo naomba elimu ya ziada!
Nimeelimika pia kutokana na elimu uliotoa hapo juu, asante!!
Under ideal conditions, maamuzi kuwa nyonga ni ndogo hivyo afanyiwe operation hutolewa na daktari; Na daktari hutoa maamuzi hayo baada ya kuwa amepima njia ya mama mjamzito, na kuona kuwa size ya nyonga ya mama ni ndogo kuliko kawaida na haitaweza kupitisha mtoto kwa njia ya kawaida. Ideally, yote haya hufanyika wakati mama mjamzito anahudhuria kliniki, na ndipo sasa daktari baada ya kumpima huamua kama mtoto anawez kupita au laah. Ndio maana ni muhimu sana kwa mama mjamzito kuweza kuhudhuria kliniki zake kama anavyopangiwa; ili haya yote yafanyike. (Pamoja na vipimo vingine vingi pia kama wingi wa damu, grupu la damu la mama, ultra saundi ya kuangalia ukuaji wa mtoto na ukubwa wa mtoto, etc).
Na pia, ni kweli kuwa mtoto anaweza kuwa mkubwa kuliko kawaida, kiasi cha kusababisha kuwa vigumu/kutokuwezekana kwa mtoto kupita katika njia ya kawaida na hivyo mama kuhitaji oparesheni (kikawaida, mtoto kuanzia kilo 4.5 huwa inakuwa vigumu kuzaliwa njia ya kawaida). Lakini, pia wako ambao wanazaa watoto hata wa kilo 5 kwa njia ya kawaida (nimeshuhudia wengi tuu); Ndio maana ni muhimu kwa vipimo kuweza kufanyika mapema; ili sasa daktari aweze kuangalia kwa kadri ya makadirio ya uzito wa mtoto yalivyofanyika (huwa inakadiriwa kwa ultra saundi), na pia kwa ukubwa wa nyonga ya mama, je huyu mama ataweza kupitisha mtoto huyo kwa njia ya kawaida?? Au atahitaji oparesheni, na kama atahitaji oparesheni, aweze kupangiwa tarehe (elective cesarean section), ili asipate leba, apigwe kisu moja kwa moja. Kwa hiyo kwa ufupi, ndio inawezekana size ya mtoto ikasababisha mama ajifungue kwa oparesheni (hasa kama ni zaidi ya kilo 4.5), na inawezekana kama mimba inayofuatia mtoto kama akiwa ni mdogo (kwa mfano kilo 3), akapita vizuri tuu.
Tatizo kibongo bongo, wamama hawahudhurii kliniki kama inavyotakiwa, na pia hata wanaohudhuria, kliniki nyingi hazina huduma zile ambazo ni standard mjamzito anatakiwa apate (kama ultra saundi), na wanalipua lipua tuu. Matokeo yake, vitu ambavyo ilibidi vijulikane mapema kabisa wakati wa kliniki vinakuja kujulikana wakati wa leba, na kusababisha heka heka na matatizo lukuki. barafuyamoto
 
Asante sana Dr., nimejifunza kitu muhimu siku ya leo mpaka sasa toka kwako!!
 
Muda gani maalum
maana wangu mi kabeba ikiwa imepita mwaka na mi 6 tangu apasuliwe.
hiyo ni risk,inakuwa vigumu kufanya trial of scar sababu inatakiwa at least miaka 3 ndio abebe mimba
 
Ewe Mwenyezi wanusuru mama zetu na janga hili la operation,
manake mh! Omba yasikukute.
 
Ipo factor nyingi za mtu kuzaa kwa oparation , lkn akizaa yakwanza ya pili anaweza kuzaa kwa kawaida isipokuw tu kama amepata mimba mapema sana chini ya mwaka mmpja laima afanyiwe elective mana ili azae kawaida anatakiwa akae miaka 3 ndo abebe mimba tena
 
Kurudiwa kwa operation ya kujifungua ni kwa sababu: kama mama ana maumbile madogo hususani ya mifupa ya nyonga au alipata kupooza nyonga akiwa bado mdogo basi huyo atahitaji kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua. Kama sababu za kufanyiwa upasuaji sio zile zinazojirudia kama kutoka damu ukeni kwenye mimba pevu, mtoto kutanguliza matako, mapigo ya mtoto kuwa kasi au kupungua katika mimba zinazofutia si lazima kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua.
Mara mama anapofanyiwa upasuaji kwa mara ya pili kwa ajili ya kujifungua basi huyo anashauriwa awe anajifungua kwa njia ya upasuaji kwani kovu lake si salama.
Asante

Maana watu wanadhani ni "kupenda" u "uvivu"
 
Jibu la swali lako ni HAPANA.
Bali, inategemea nini hasa kilisababisha "oparesheni" katika huo uzao wa kwanza? Kama ni sababu ambayo ni permanent na haibadiliki, basi ndio hataweza tena kujifungua njia ya kawaida (mfano: njia ya uzazi "nyonga" ndogo isiyoweza kupitisha mtoto). Kwa hiyo basi, kama uzazi wa kwanza ulijifungua kwa mnjia ya oparesheni, na sababu ilikuwa ni ile ambayo sio ya permanent mfano kondo kutangulia (placenta previa), uzazi wa pili unaweza kujaribu kujifungua kwa kawaida (trial of scar). Lakini, hii inabidi ifanyike chini ya uangalizi, kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya wamejiandaa kufanya oparasheni muda wowote ule mambo yakienda vibaya.
Baadi ya sababu ambazo zinaweza kusababisha ushindwe kujifungua njia ya kawaida na kuhitaji "oparesheni" ni kama ifuatavyo:
-Nyonga nyembamba isiyoweza kupitisha mtoto
-Kama una ugonjwa mwingine wa muda mrefu ambao utaleta shida wakati wa kujifungua kama ugonjwa wa moyo,
-Mtoto kutanguliza miguu/matako
-Kondo kutangulia (placenta previa)
-Mtoto mkubwa kupita kiasi (big baby)
-Mimba ya mapacha wawili/watatu/wanne
-mtoto kulala vibaya (transverse/oblique lie)
-Uchungu kwenda taratibu sana au kushindwa kuprogress
-Mtoto kuchoka (fetal distress).
Ni muhimu kuelewa kuwa, sababu zote hizo hapo juu (isipokuwa ya kwanza), ni sababu ambazo ni relative; kumaanisha kwamba si lazima mfano mama akiwa na mimba ya mapacha basi ajifungue kwa oparesheni, uamuzi utategemea mambo mengi ikiwa ni pamoja na hali ya mama,etc etc.
Abuu Ibrah
Asante dr....
 
Back
Top Bottom