Pre GE2025 Je, ni kweli Mungu hana Demokrasia? Mbona alisema "Tufanye mtu kwa mfano wetu"

Pre GE2025 Je, ni kweli Mungu hana Demokrasia? Mbona alisema "Tufanye mtu kwa mfano wetu"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nauliza tu baada ya kumsikia RC Makonda akisema Mungu hana Demokrasia. Mwanzo 1:26 - Tufanye mtu kwa mfano wetu.

Je, ni kweli?

Nawatakia Dominica njema 🌹

=====

RC Makonda atahadharisha akuhusu walaghai wanaotumia neno la Mungu kurubuni wananchi

Akizungumza na maelfu ya Wananchi wanaohudhuria Kongamano kubwa la Operesheni Washa Taa linaloratibiwa na Mtume Boniface Mwamposa wa Kanisa la Inuka Uangaze, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka watanzania kuwakataa watu wanaotumia Neno la Mungu na mavazi rasmi ya Viongozi wa dini katika kuwarubuni Watanzania na kujinufaisha kupitia maandiko matakatifu.

"Ukimuona mtu yeyote mwenye jina au nafasi yoyote ya kidini lakini umaarufu wake hautokani na kazi ya mikono ya Kristo, hautokani na kazi za Mungu na za neno la Mungu, jua huyo ni Kiongozi wa dini feki. Nikupe mfano unielewe, Apostle Mwamposa hapa kamtaja Yesu Mwanzo mpaka mwisho, mmejaa hapa mnashuhudia kazi za neno la Mungu kupitia kinywa cha Mtumishi wake aliyepakwa mafuta kwaajili ya nyakati hizi, Heshima aliyonayo ni ya kufanya kazi ya Mungu ambayo sisi ni mashuhuda wa Matunda na maandiko yanasema mtawajua kwa matunda yao." Amesema Mhe. Makonda.

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mhe. Makonda amewaambia watanzania kuwa kumekuwepo na lindi kubwa la wanaojiita watumishi wa Mungu sasa hivi wakiwa na ukwasi na majina maarufu lakini umaarufu wao hautokani na kazi ya Uponyaji na kazi za mikono ya Kristo kama ambavyo kanuni zinazungumza kuhusu wakristo na Ukristo ulimwenguni kote.

Katika kudhihirisha uhakika wa kile alichokizungumza, Mhe. Paul Christian Makonda amealika na kuwakaribisha watu wanaohitaji mjadala naye kuhusu Ukristo, namna inavyotakiwa maisha ya mkristo kuwa pamoja na namna mbalimbali ambazo Mungu ameagiza na kuelekeza Wakristo katika utatuzi wa changamoto za kijamii na namna wanavyotakiwa kuishi wao pamoja na Viongozi wao wa kidini.
 
Kwa hiyo kifupi, DAB kama mkuu wa magenge ya uuaji hataki demokrasia?
 
Mungu kutuumba na nafsi huru tuamue tutakayo ndio demokrasia kuu na msingi wa demokrasia zote.
 
Nauliza tu baada ya kumsikia RC Makonda akisema Mungu hana Demokrasia

Je, ni kweli?

Nawatakia Dominica njema 🌹
Katika Qur'ani, kuna maelezo yanayoelezea kuhusu uhuru wa imani na kila mtu kuwa na dini yake.

Mojawapo ya aya maarufu inayozungumzia uhuru wa dini ni Surah Al-Kafirun (109:6), ambapo Allah anasema:

"Nyinyi mna dini yenu, nami nina dini yangu." (109:6)Aya hii inaonyesha kuwa kila mtu anaruhusiwa kufuata imani yake, na hakuna kulazimishwa katika masuala ya dini.

Aidha, aya hii inasisitiza kuheshimu tofauti za kidini kati ya watu.Pia, katika Surah Al-Baqarah (2:256), Qur'ani inasema:"Hakuna kulazimishwa katika Dini..." (2:256)

HII DEMOKRASIA. UCHAGUE NURU YAANI UISLAMU AU UCHAGUE GIZA USIOKUWA UISLAMU
 
HII DEMOKRASIA
Hii uongo mbana islamic states hawaruhusi dini zingine
 
Hii uongo mbana islamic states hawaruhusi dini zingine
Islamic staste mimi nawasikia wamagharibi tu ktk media zao, ktk Quran hawahaandikwa jina hilo. Any way Hata Vatican mle hukuti sheikh wote wakiristo tu na ukisema vizuri uislam unaweza ukafukuzwq upadri
 
Katika Qur'ani, kuna maelezo yanayoelezea kuhusu uhuru wa imani na kila mtu kuwa na dini yake.

Mojawapo ya aya maarufu inayozungumzia uhuru wa dini ni Surah Al-Kafirun (109:6), ambapo Allah anasema:

"Nyinyi mna dini yenu, nami nina dini yangu." (109:6)Aya hii inaonyesha kuwa kila mtu anaruhusiwa kufuata imani yake, na hakuna kulazimishwa katika masuala ya dini.

Aidha, aya hii inasisitiza kuheshimu tofauti za kidini kati ya watu.Pia, katika Surah Al-Baqarah (2:256), Qur'ani inasema:"Hakuna kulazimishwa katika Dini..." (2:256)

HII DEMOKRASIA. UCHAGUE NURU YAANI UISLAMU AU UCHAGUE GIZA USIOKUWA UISLAMU
😂😂😂
 
Kama ni kuota mkia basi huu wa makonda umezidi.Hakuna mtu wa mfano kwenye demokrasia kama Mungu na nakwambia kama Mungu angekuwa dikiteta mafwele na huyu makonda wasingekuwa wanaishi na ata shetani angekuwa ameshateketezwa lakini demokrasia ya Mungu inawafanya leo wanaishi. kinyume cha demokrasia ni uchawi na umasikini na kamwe huwezi kuwa na maisha bora ata siku moja.Ndo maana ili makonda na wenzake wapate mkate wao mpaka waue watu au waharibie wengine maisha huu sio umasikini bali ni ufukara.
 
Bashite kachemka,Ile ukimuomba na Akasamehe dhambi zako na kukupa Neema mpya kwenye maisha tayari ni Democrasia. Mwembieni Mungu halinganishwe/unquestionable.
 
Back
Top Bottom