Je, ni kweli nyumba mnazoziita contemporary (Hidden roof ) zinapunguza gharama ya kupaua?

mafundi washakula hela ya ufundi huwaoni tena

Nililala lodge yakuitwa Password, Tabata Segerea, ndani iko poa kinoma nilishangaa kuona gypsum boards zote ziko tepetepe

asubuhi natoka nachungulia juu naona ni huo mtindo wa roof, nikasema kayakanyaga
[emoji1][emoji1]
 
Sasa wewe unaongelea upauaji wa mafundi wasiojua kupaua. Ukipaua inavyotakiwa bati haichimbiwi kwenye tofali wala haiwekwi mortar. Kuna chemical inaitwa synroof inapakwa, kwenye bati na ukuta vinapokutana, then kuna membrane inawekwa juu ya hiyo synroof halafu unapaka tena synroof juu yake.

NB: Mimi siyo fundi na wala picture siyo ya kwangu
 

Attachments

  • dutan_housing_20200930_2.jpg
    76.6 KB · Views: 66
Me nasema hizi nyumba ni fashion kama yalivyo mavazi tu.

Kuokoa gharama za bati na mbao, tuseme paa hazikusaidii kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba nzima.

Tena hizi ni nyumba ghali sana kuzidi hizi za kawaida.
 
Gharama ni ile ile au inaweza kuongezeka maana contemporary unapunguza gharama za mbao na mabati lakini unaongeza gharama za cement , matofali , water proofing chemical ( gallon moja ni laki mbili na nusu) na inaongeza nondo za rinta na nondo za mifereji ukizingatia bei ya nondo sasa hivi inaweza kuzidi kuliko roof ya kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…