KWELI Je ni kweli raia nchini urusi wanakimbia maeneo ya crimea kukwepa mashambulizi ya urusi?

KWELI Je ni kweli raia nchini urusi wanakimbia maeneo ya crimea kukwepa mashambulizi ya urusi?

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
kumekuwepo na picha ambayo imechapishwa kwenye mtandao wa facebook ikiwa na nukuu ya kuwa raia wa urusi wanaondoka eneno la crimea kwa huhofia mashambulizi ya urusi

katika chapisho hilo ambalo linaonekana kuwana nukuu ifuatayo “Hali ya usalama katika mkoa wa Crimea imezidi kuwa mbaya kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Ukraine dhidi ya miundombinu ya kijeshi na nishati.

Katika chapisho hilo imedai kuwa foleni kubwa zimejitokeza kwenye njia za kutoka katika mkoa wa Crimea huku baadhi ya magari yakiachwa njia baada ya kuishiwa mafuta, wakati sehemu kadhaa zikiripotiwa kukumbwa shida kubwa ya kukatika kwa umeme.
CRIMEA.jpg
 
Tunachokijua
Foleni Kubwa za Magari, Kuna ukweli kwamba kumeshuhudiwa misongamano mikubwa ya magari (wakati mwingine hadi urefu wa kilomita 10 hadi 15) kwenye maeneo ya kukagua usalama kuelekea Daraja la Kerch (Crimean Bridge) linalounganisha rasi hiyo na Urusi. Raia wengi, wakiwemo watalii na wakazi wa Urusi waliohamia huko, wamekuwa wakijaribu kuondoka rasi hiyo.

Raia wengi wamekuwa wakiondoka kutokana na hofu ya kuongezeka kwa mashambulizi ya droni na makombora kutoka kwa jeshi la Ukraine, ambayo yanalenga miundombinu ya kijeshi na usafirishaji ya Urusi eneo hilo.

Mbali na mashambulizi, kuondoka kwa raia kumesababishwa pia na kukatika kwa umeme mara kwa mara pamoja na uhaba mkubwa wa mafuta uliotokana na Ukraine kufanikiwa kukata njia muhimu za usambazaji wa vifaa vya vifaa vya kiulinzi na kijeshi (Logistics Lockdown).

Picha inayotumika inaonyesha msongamano mkubwa wa magari kwenye Daraja la Kerch ambapo namba za usajili za magari hayo (kama vile zenye kanda ya Moscow - 190/90) zinathibitisha kuwa ni raia wa Urusi.

Matukio ya foleni ndefu kama hii yamekuwa yakijirudia kila pale Ukraine inapozidisha mashambulizi au kukiwa na tishio la droni, ambapo mamlaka za Urusi zinalazimika kufunga daraja hilo kwa saa kadhaa kufanya ukaguzi mkali wa kiusalama, na kusababisha msongamano mkubwa wa magari yanayotaka kukimbilia upande wa Urusi bara.​
Back
Top Bottom