Je, ni kweli Sekta Binafsi inasaidia kukuza Uchumi?

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Mikopo inayotolewa kwa sekta binafsi imezidi kuongezeka kutoka 7.8% mwaka 2021 hadi 22.5% mwaka 2022 pia imeongezeka zaidi hadi kufikia january 2023 imefikia 23.1%. Hii inaashiria kuimarika kwa uchumi na utendaji wa sekta binafsi unaochagizwa na sera bora za serikali ya Rais Samia Suluhu.

Lakini pia Rais Samia Suluhu anaendelea kusisitiza kushilikiana kwa sekta binafsi na serikali maana anajua kuwa sekta binafsi inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi na inasaidia kupunguza tatizo la ajira Tanzania.

"Maendeleo makubwa na ya haraka yanapatikana kwa kufanya kazi na sekta binafsi ya ndani na ya kimataifa. Kutambua hilo, viongozi tuhakikishe ofisi tunazoziongoza zinakuwa wezeshi na sio vikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji." Alisema Rais Samia Suluhu.
 
Sasa mzee unauliza umuhim wa dawa kwa mgonjwa?

Hata hivo kuongezeka Mikopo sio indicator nzur ya uchumi kuimarika, maana hiyo mikopo inaweza kuja kuwa NPLs bank zikayumba....
 
Idadi ya watu walioajiriwa na serikali mpk leo hii haijafikia 1M, lkn kwenye sekta binafsi wanakimbilia 5M. Tafakari.
 
Mikopo inayotolewa kwa sekta binafsi imezidi kuongezeka kutoka 7.8% mwaka 2021 hadi 22.5% mwaka 2022 pia imeongezeka zaidi hadi kufikia january 2023 imefikia 23.1%. Hii inaashiria kuimarika kwa uchumi na utendaji wa sekta binafsi unaochagizwa na sera bora za serikali ya Rais Samia Suluhu.

Lakini pia Rais Samia Suluhu anaendelea kusisitiza kushilikiana kwa sekta binafsi na serikali maana anajua kuwa sekta binafsi inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi na inasaidia kupunguza tatizo la ajira Tanzania.

"Maendeleo makubwa na ya haraka yanapatikana kwa kufanya kazi na sekta binafsi ya ndani na ya kimataifa. Kutambua hilo, viongozi tuhakikishe ofisi tunazoziongoza zinakuwa wezeshi na sio vikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji." Alisema Rais Samia Suluhu.
Nashangaa sana kuona mada kama hii ipo huku imepoa kabisa bila wachangiaji wa kutosha.

Hii ni aina ya mada moja mhimu sana, lakini wachangiaji naona hatuioni hivyo, sijui kwa nini?

Maoni yangu kwa ufupi kwa sasa, ni kuwa sehemu zote, binafsi na za kijamii ni muhimu katika maendeleo; lakini hizi nyimbo tunazoimbishwa na wakubwa sasa hivi kuihusu sekta binafsi ni wazi kwamba tunarudishwa kwenye utegemezi na kubaki huko milele. Angalau hata ingekuwa hiyo "binafsi" ni inayotuhusu sisi, wananchi wetu wenyewe ili wawezeshwe na kupanua wigo wao zaidi; lakini ukifuatilia "binafsi" inayopigiwa chapuo zaidi na kuwezeshwa, ni hao hao waliowahi kututawala. Kwa nini tusiseme wanarudi kupitia mlango wa uani kututawala zaidi.
Ukikataa wanayoyahimiza wao, kama "ushoga", wanakutandika kama walivyomtandika Mgabe na wanaendelea kuwakandamiza wananchi wa Zimbabwe kwa vikwazo vya kiuchumi.
 
Kuwezeshwa kupi huko unako kutaka ambako kuna kosekana? Mimi nadhani sisi wazawa tusibweteke tukisubiri kuwezeshwa. Serikali kazi yake ni kuweka mazingira mazuri ya kusaidia kukuza sekta binafsi...then sisi tunapaswa kuchangamkia fursa
 
Sikubaliane na wewe, kama huelewi maana ya kuwawezesha wananchi kushika hatamu ya maendeleo yao.

Hata kutoa elimu tu au taarifa ziwafikie wananchi ni uwezeshaji. Kama wewe hujui hilo utakuwa na matatizo.

Na huko unakokuita wewe "kubweteka" bado huoni mchango wa serikali katika tatizo hilo? Panua akili uwe na upeo, siyo kulaumu tu bila kujua msingi wa lawama hizo ni nini hasa!
 
Kuwezeshwa kupi huko unako kutaka ambako kuna kosekana? Mimi nadhani sisi wazawa tusibweteke tukisubiri kuwezeshwa. Serikali kazi yake ni kuweka mazingira mazuri ya kusaidia kukuza sekta binafsi...then sisi tunapaswa kuchangamkia fursa
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa. Tatizo kubwa linalotusumbua sasa hivi ni la uelewa. Wananchi wetu wengi bado wana mtazamo wa kiujamaa, wakiiangalia serikali ifanye mambo, wakati enzi za ujamaa zimeshapita na sasa ni wakati wa wanannchi kufanya mambo. Kama ulivyosema, kazi ya serikali ni kuweka mazingara mazuri ya kuwezesha sekta binafsi kustawi; lakini utashangaa bado kuna watu wanaitazama serikali na kutaka iwafanyie mambo!
Ni wajibu wetu sisi wananchi kutumia elimu, mazingira, ubora wa mawasiliano, nk, kutambua fulsa zilizopo na kuzichangamkia. Tukisubiri serikali itufanyie itakula kwetu, na tutabaki kulalamika na kulaumu siku zote.
 
Idadi ya watu walioajiriwa na serikali mpk leo hii haijafikia 1M, lkn kwenye sekta binafsi wanakimbilia 5M. Tafakari.
Hao wa sekta binafsi wengi ni vibarua tu wasiochangia hata NSSF
 
Back
Top Bottom