SI KWELI Je, ni kweli taarifa hii ya kukemea uchawa imetolewa na UVCCM Momba?

SI KWELI Je, ni kweli taarifa hii ya kukemea uchawa imetolewa na UVCCM Momba?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
photo_2026-05-08_16-44-36.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na taarifa inayodaiwa kutolewa na Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM)
Wilaya ya Momba na ikikemea tabia ya uchawa kwa vijana na kwamba tabia hiyo huondoa ukweli, huharibu misingi ya uwajibikaji na kudhoofisha uwezo wa vijana kuwa viongozi wa kesho wenye maadili na uwezo wa kusimamia ukweli.

Aidha taarifa hiyo inahitimisha kwa kubainisha kuwa chama kinahitaji vijana wenye maono, uadilifu na ujasiri wa kusimamia ukweli. Uchawa haujengi chama wala Taifa; hujenga watu binafsi kwa muda mfupi. Kijana mwenye heshima ni yule anayesimamia ukweli, anafanya kazi kwa bidii na anaitumikia jamii kwa moyo wa uzalendo na uwajibikaji.


Lakini Je, nikweli taarifa hiyo imetolewa na UVCCM Momba?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani haijatolewa na UVCCM Wilaya ya Momba kama inavyoonekana kwenye taarifa hiyo. Vilevile muundo wa barua hiyo haufuati muundo rasmi ambao umekuwa ukitumiwa katika taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na UVCCM.

Sanjari na hayo Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM taifa Mohammed Kawaida ameikana barua na kwamba haijatolewa na UVCCM.​
Back
Top Bottom