Je, ni Kweli Tanzania tunaitegemea Kenya? Siyo Kweli

Je, ni Kweli Tanzania tunaitegemea Kenya? Siyo Kweli

Khalid Sankara

New Member
Joined
Nov 3, 2021
Posts
4
Reaction score
21
Biashara kati ya Tanzania na Kenya imekuwa ikikuwa kwa kiwango flani kutokana na uwepo wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyoanza mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Tangu kipindi cha kuundwa kwa jumuiya hiyo , biashara imekuwa ikikuwa na mpaka kufika 2021, biashara kati ya Tanzania na Kenya imefika Dola Billioni 1 ( zaidi ya trillioni 2).

Lakini katika kipindi kikubwa cha miaka hii 22, Kenya ndiyo inaonekana ikinufaika zaidi. Sababu kuu ya Kenya kunufaika zaidi ni kutokana na uwepo wa viwanda vingi vya bidhaa za viwanda, na rasilimali watu.

Je Tanzania tunategemea nini kutoka Kenya?
- Kwa kiwango kikubwa bidhaa nyingi tunazotegemea nchini Kenya ni bidhaa za viwandani kama madawa, kemikali, processed food products n.k.

-Kwa upande wa Kenya , wao wanaitegemea zaidi Tanzania kwa mazao na matunda , pamoja na soko la utalii, ajira kwa raia wake n.k.

Je ni kweli Tanzania tunaitegemea Kenya au ni Kenya ndiyo inaitegemea Tanzania ?.
- Ni kweli kwa kiwango flani bidhaa ndogo ndogo nyingi za viwanda nyingi zipatikanazo nchini hutokea Kenya.
Na pia Kenya ni soko kubwa la mazao na matunda nchini.

Lakini ukweli ni kwamba bidhaa hizi nyingi zitokazo Kenya,hupatikana kwa bei rahisi nchini Afrika Kusini na nchi nyengine za kusini mwa Afrika.

Hii kutokana na maendeleo makubwa ya nchi hiyo. Miongoni mwa sababu zinazofanya bidhaa hizo kupatikana kwa bei nafuu nchini humo ni ; kuendelea kwa viwanda vyake, uchumi mkubwa , gharama ndogo za uzalishaji na usafirishaji.

Hivyo, Kenya analihitaji zaidi soko la Tanzania kuliko Tanzania inavyohitaji bidhaa za Kenya.
-Tukija kwenye upande wa utalii, Kwa miaka mingi Wa Tanzania wengi wamekuwa wakilalamika juu ya upotoshaji wa vivutio vya utalii nchini ( kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro), kutangazwa vinapatikana Kenya.

Jambo hili lilikuwa halifanywi kwa bahati mbaya. Kwani vivutio vya utalii vya Tanzania ndiyo maarufu zaidi Duniani kwa ukanda wa Afrika Mashariki, na Tanzania ndiyo nchi yenye vivutio vya utalii vingi zaidi barani Afrika na ya pili Duniani baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii.

Kwa kuwa Kenya walishalitambua hilo, miongoni mwa mbinu waliyoamua kutumia ili kuchukua baadhi ya watalii wenye lengo la kutembelea Tanzania ni kutangaza vivutio hivyo vipo Kenya, na kutaka Afrika Mashariki iwe na visa mmoja ya utalii.

Baada ya juhudi mbalimbali za kukomesha upotoshaji wa taarifa za vivutio vya utalii vya Tanzania.
Idadi ya watalii na mapato yanayotokana na utalii nchini Tanzania yameongezeka mara dufu huko yale ya Kenya, huu ni ushahidi tosha Tanzania ilikuwa ikipoteza mapato mengi ya utalii kutokana na upotoshaji uliokuwa unafanywa hapo awali.

Mwaka 2018 matunda ya kukomesha upotoshaji wa taarifa za vivutio vya utalii na utangazaji wa vivutio vya utalii nchini yakaanza kuonekana, na mwaka 2019 mapato ya utalii Tanzania yalikuwa Dola Billioni 2.4 karibu mara mbili ya Kenya ( Dola Billioni 1.3), na tangia kipindi hicho Kenya haijawahi izidi Tanzania kwa mapato ya utalii.

Huku mwaka 2020 , Tanzania ikiingiza mapato ya utalii mara nne zaidi ya Kenya.
-Tukienda kwenye mazao na matunda, Kenya ndiyo mnunuzi wa mazao haya kwa nchi za Afrika.
Lakini sii kweli Kenya ndiyo mhiitaji pekee wa mazao haya. Kwani kwa hali ilivyo sasa karibu robo ya bara la Afrika lina janga la njaa.

Huku nchi kama Ethiopia, Somalia, Afrika ya Kati, Chad, Sudan , Sudani Kusini n.k zikiwa katika hali ya hatari. Na huko mbeleni kutokana na nchi za Afrika kutozalisha vyakula kwa kipindi cha miaka 2, kuna hatihati ya nchi nyingi za Afrika kukukmbwa na janga la njaa. Hii inamaanisha theorotically Tanzania teyari inasoko jipya la watu bilioni 1.

Hivyo basi, changamoto ya soko la mazao ya vyakula kwa Tanzania ni ndogo.
- Kwa upande wa ajira hilo lipo wazi kwani ripoti ya hivi karibuni ya remittances ya nchini Kenya, inaonyesha raia wa Kenya waishio nchini Tanzania ndio walio ongoza kurudisha pesa nyingi nchini Kenya (remittances) , kwa wakenya waiishio bara la Afrika.

Hili limechangiwa kwa kiwango flani na Tanzania kulegeza baadhi ya mashariti ya kuajiliwa nchini kwa raia wakigeni.

Hizi ni baadhi tu ya sababu tu, kwa nini Tanzania siyo tegemezi kwa Kenya.
 
Back
Top Bottom