Wasanii wetu wa muziki wa kizazi kipya huwa hawaishiwi mambo na majambo.
Ni muda mrefu sasa tumekuwa tukisikia Q Chief akimtuhumu kwenye vyombo vya habari T.I.D kuwa ndiye anayeisiliba nyota yake ya kuwika.
Swali la kujiuliza ni hili, mbona naye T. I. D hawiki kama zamani? Je ni nani anayemroga?
Mi nadhani mchawi wao wenyewe. Kila mtu anajiroga kwa kurika na mafanikio kidogo waliyoyapata huko nyuma, wakavimbisha vichwa na kulemaa.
Sasa imeibuka damu changa ambayo iko very creative, wanamasauti hao na ma style ya kufa mtu.
Wabadilike wakaze msuli watatoka. Waache kusingizia na kupakazuiana uchawi.
Urozi ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa baadhi ya wabongo!...Akiugua anawaza kurogwa, akishindwa kuachieve kitu anawaza urozi...Labda anamroga kwa mbinu za kisasa na mipangilio mizuri ya kikundi chake!
ni heri mtu ufilisike pesa na mali, lakini si akili, hekima na mtazamo, mi nadhani nyakati zimeish wapita, sasa wanatapatapa tu ili wawe karibu na waandishi wa habari
ni heri mtu ufilisike pesa na mali, lakini si akili, hekima na mtazamo, mi nadhani nyakati zimeish wapita, sasa wanatapatapa tu ili wawe karibu na waandishi wa habari
Walidhani kubakia juu mchezo?
Kukwea juu si kazi kazi ni ku sustain.
Ulozi ni kisingizio au ni sababu ya haraka wanaoitumia kujitetea kwanini wamefulia.