- Source #1
- View Source #1
Je, ni kweli Trump ali-react baada ya kusikia 'Allahu Akbar' wakati wa hotuba yake?
- Tunachokijua
- Donald John Trump ni mwanasiasa wa Marekani, na mfanyabiashara ambaye ni rais wa 47 wa Marekani. Akiwa mwanachama wa Chama cha Republican, alihudumu pia kama rais wa 45 kuanzia 2017 hadi 2021.
Madai
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwapo na kipande cha video kinachomuonesha Rais wa Marekani Donald Trump akiwa anakimbia kutoka jukwaani na kudaiwa ni kutokana na sauti ya Allahu Akbar iliyosikika katika eneo hilo.
Uhalisia wa video hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa video hiyo ni halisi lakini imehaririwa sauti kwa kuwekewa sauti ambayo haikuwepo katika tukio halisi.
Tukio halisi lilitokea Machi 12, 2016 wakati Donald Trump akiwa kwenye kampeni za uchaguzi wa Urais kuelekea awamu yake ya kwanza ambapo wakati akihutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jijini Ohio siku ya Jumamosi. Ambapo mwanaume mmoja aitwaye Thomas Dimassimo alijaribu kukimbilia jukwaani lakini baadaye alikamatwa na kushtakiwa kwa mwenendo mbaya na kusababisha hofu.
Kulingana na shahidi Chris Famiano wa Columbus alieleza kuwa "Trump alikuwa akitoa hotuba yake na kila mtu alikuwa ndani yake. Na ndani ya sekunde moja mtu kutoka karibu na bend alikuwa ameruka juu ya uzio huku akimshtaki Donald Trump.