Je, ni kweli viporo vya chakula vinadumaza watoto?

Je, ni kweli viporo vya chakula vinadumaza watoto?

Riskytaker

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2024
Posts
568
Reaction score
2,522
Je, ni kweli viporo vinadumaza mwili na akili.

1676389990311.jpg
 
hivyo viporo kama vina mpangilio mzuri wa kula sizani kama ni tatizo. africa ya mashariki tumejaliwa kua na vyakula vya kila aina.tatizo kula hatujui.(mpangilio wa vyakula hakuna) kingine hii dhana ya manesi na madokta kuwaambia wamama wasiwape kitukingine watoto hadi miezi 6 sio dhana nzuri.
mama anajifungua bila kujua anafuata alichoambiwa na dk kua anyonyeshe tu wakati anajua huyo mama hana afya ya kutosha na hata maziwa yake sio mengi ya kutosha na hayana virutubisha vya kutosha vya kumjenga mtoto. naamini hii ndio sababu ya watoto kudumaa.
mtu mwenye kipato kizuri ananunua maziwa ya ziada.lakini kama huna kipato sio lahisi kununua maziwa ya kopo maana bei ni kubwa.
WATOTO WANADUMAA KWASABABU YA KUKOSA CHAKULA BORA TANGU UTOTONI. KUANZIA KWA MAMA HADI KWENYE UKUAJI WAKE.
 
Viporo vya wa Watanzania vingi ni starch tupu

Starch ya viporo na mkate mweupe vyote vinadumaza mwili na akili ya Watoto wa kiafrica

Ndio maana watoto wengi wa kiafrika hawajiamini, hawako courageous na ni wajinga wajinga, usomi wao ni kujua kiingereza tu

Tazama watoto wa kichina, kijapan na Wahindi wa sasa...wapo vizuri

Kuls vuporo watoto wanaishia kujambajamba tu hovyo lakini cognitively hamna kitu

Tena Ugali ndio haufai kabisa
 
Ninachosikia sana kuhusu viporo ni kwamba vinaweza kuleta maambukizi ya bacteria,

Sasa kwa hiyo picha unataka kusema iringa inadumaza sana watoto kwasababu inaongoza kwa kula viporo?

Umejuaje inaongoza?

Labda huko watu wanakula sana wanga, mboga kidogo

Au ni vile kumejaa wabena na wahehe, wafupi kwa asili😅
 
Je, ni kweli viporo vinadumaza mwili na akili.

Huu ni uzushi mtupu kabisa. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wametoa hizo Takwimu (graph) 👆👆lakini haijatoa visababishi (causes)vya kuwepo kwa hali hiyo ya Udumavu kwamba ni kutokana na ulaji wa kiporo.
Inafaa mtoa mada ukumbuke kwamba HAKUNA mtu yeyote asiyekula kiporo - Hakuna. Awe mkubwa, mdogo, tajiri, maskini, mweupe au mweusi Wote ni mtindo mmoja - Wanakula viporo.
Labda nikuulize hivi; Mikate unayokula unajua imekaa dukani muda gani? Soda, juice, beer, maziwa ya supermarket, samaki, dagaa ndo usiseme kabisa n.k. n.k. vyote ni viporo kwa maana ya kiporo ni chakula kilicholala au kilichokaa kwa siku moja au zaidi toka kiandaliwe. Tusidanganye hapa eti wamedumaa kwa sababu ya ulaji wa viporo.:AYAYASip: Tafuta sababu nyingine bro.
 
Back
Top Bottom