je ni kweli vyuo vyetu vikuu (tanzania) ni ngumu kupata "a'' ukilinganisha na nchi zilizoendelea ?

2013

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
11,360
Reaction score
6,069
ningependa kuiweka hii topic kihivyo kwasababu mimi ni mgeni kidogo hivyo basi sijajua kama hii topic imewahi kugusiwa huko nyuma ama la. kimsingi nataka nipate maoni yenu wasomi na waalim na wengineo kwa ujumla juu ya madai kuwa hapa nchini lecturers(wakufunzi wa chuo ) wengi wanabana kutoa alama za A katika masomo, na kama mpo mia moja basi wanaweza kuwa watu nane tu ndo wanaishia kupata A wengine wanachezea makarai (yaani alama ya C) kama ni kweli nini hasa chanzo cha hili tatizo katika kuiboresha elimu yetu nchini. na pia nilipata tetesi kuwa nchi zilizoendelea huwa hakuna tatizo hili. kama lipo je tatizo ni lecturer wanafunzi wetu wanaotakiwa kulaumiwa au mfumo? asante:A S check_03::A S check_03::A S check_03::A S check_03::A S check_03:
 

Sidhani kama kuna ukweli wowote. Kwanza huko majuu kwenyewe inategemea na kutofautiana baina ya taasisi na taasisi.

Kwa mfano, huwezi kulinganisha grading ya DeVry University au University of Phoenix na Emory University au Cornell University.

Sasa hebu jiulize, unaweza kweli kulinganisha Emory au Cornell na UDSM au Mzumbe?
 
Kuna ukweli kiasi fulani, kwa mfano kwa nchi nyingine ukifanya mtihani then let say ukapata B plan na kama hukubaliani na matokeo waweza omba mtihani mwingine na ukifaulu ukipata A then ndo yanakuwa matokeo yako tofauti na bongo!

Huo ni mfano nadhani wadau wengine wana mifano mingi zaidi
 

vilaza ndiyo huwa wanaamini katika kubaniwa. Hivi mwalimu akubanie ili iweje? Nadeclare interest, mimi ni mwalimu wa college, haya madudu wanayoniandikia sidhani kama kuna atakayekuja kupata A, kila siku wanalalama eti nawabania licha ya kwamba hakuna aliyethubutu kuappeal hata siku moja...
 
''Ukiona nimempa mwanafunzi 'A' ujue kwenye insha yake kuna kitu kipya nimejifunza'' by Prof.Mukandara.profesor of political science and public administration Udsm.
 
''Ukiona nimempa mwanafunzi 'A' ujue kwenye insha yake kuna kitu kipya nimejifunza'' by Prof.Mukandara.profesor of political science and public administration Udsm.

ndiyo yupo sahihi, mtihani siyo kuhamisha points na maelezo kama yalivyo
 
Kupata A inamaanisha unaweza kuitetea hiyi A yako kwa mdomo na kwa maandishi. Wanavyuo ninavyowaua hata lugha ya kuandikia insha ni tatizo. Pili, hata kama mwanafunzi ameandika vizuri, huwa amenukuu maneno aliyofundishwa na mwalimu kwenye mhadhara, yaani hajaongeza chochote. Nakumbuka kuna mwalimu mmoja alitoa A nyingi kiasi kwamba hata wakaguzi wa nje wakamwonya.Je ikiwa kama hakuna ubunifu upewe A ya nini? Kumbuka alama zinatafutwa, si zinachukuliwa kama wanavyijisema "nachukua shahada ya sheria".
 

Hapana si kweli kabisa, kupata A ni jitihada zako sio mwalimu kugawa...A haipewi inatafutwa...hata UK kupata A ni mpaka kweli uwe na uwezo wa mtu wa A si kirahisi rahisi....pia inategemea na vyuo....mfano vyuo vya marekani elimu yao ni rahisi kidogo uki compare na ya UK so unakuta integration za watu wa marekani mwaka wa kwanza ni tofauti na za wa mwaka wa kwanza UK
 
''Ukiona nimempa mwanafunzi 'A' ujue kwenye insha yake kuna kitu kipya nimejifunza'' by Prof.Mukandara.profesor of political science and public administration Udsm.

Umekariri wewe ni Dr. Bana ndio husema hvyo....
 

NN utaanzisha vita hapa jukwaani na watu wa DeVry, University of Phoenix ama Strayer. Shauri zako
 
Ndo ujiulize kwanini mtanzania akienda kusoma ulaya anakuwa kichwa sana kimarks kuliko hapa
 
''a'' huwezi kupata kama unalala baa,
''a'' huwezi ukapata kama huhudhurii lekcha,
''a'' huwezi ukapata kama you don't recall what you learn
''a'' huwezi kupata kama huna mpenzi ambaye ndiye LIBRARY
''a'' huwezi kupata kama unasaini kozi weki ndogo
''a'' huwe kupata kama hujajiandaa kikamilifu na UE (University Examination)
Written by:Mbwilo,S.-from SAUT-MTWARA
 
''a'' huwezi kupata kama unalala baa,
''a'' huwezi ukapata kama huhudhurii lekcha,
''a'' huwezi ukapata kama you don't recall what you learn
''a'' huwezi kupata kama huna mpenzi ambaye ndiye LIBRARY
''a'' huwezi kupata kama unasaini kozi weki ndogozi
''a'' huwe kupata hujajiandaa kikamilifu na UE (University Examination)
Written by:Mbwilo,S.-from SAUT-MTWARA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…