Je ni kweli wajenzi wa zamani walikuwa na uwezo wa kubuni na kuunda kwa ustadi na ufanisi mkubwa kuliko wa sasa?

Kama nimemuelewa mleta mada anachozungumzia yeye ni ile "workmanship" kwa maana ya nakshi nakshi za kupendezesha hayo majengo, na sio ukubwa/urefu wa jengo
Wewe hujatembea ndio maana unasema majengo ya zamani yanapendeza kuliko ya Sasa hivi mpo serious kweli halafu kwanini mnaushamba wa kusifia vitu vya zamani hata kama havina hiyo sifa
 
Huyo boya aliejenga hilo jengo lenye rangi ya yanga mali siyo yangu ila nikikutana nae nisipozuiwa naweza kumuua
Hilo ni sawa na haya majengo ya sikuhizi ambayo juu hayana paa, ndani kunavuja mwanzo mwisho
 
Majengo ya zamani hata ukiyakuta kwenye mitaa yetu ni noma ukigonga ukuta msumali unapinda utadhani ukuta wa zege kumbe wala!

Zamani nadhani wajenzi huru (freemasons) walikuwa bado wanatumia sana teknolojia yao na ilikuwa imesambaa. Sasa wameingia wajuaji wameharibu na usomi wao
 
Halafu kuna ngoma hii hapa, kwanza umeona urefu wa hizo nguzo?

View attachment 3071250
Durable, hapo imehimili matetemeko ya ardhi ya miaka kwa miaka ,jua na Mvua lakini still ukuta hauna cracks na nguzo ziko kama zimemiminwa jana

Kwa Italy, Architect wa zamani walitumia Limestone, Miamba ya Volcano(Volcanic rocks) na materials mengine katika ujenzi
 
Kuhusu gharama za ujenzi, sahivi gharama ni kubwa kwani kuna matumizi ya mashine na vifaa vingine, lakini zamani walitumia mikono na nguvu kazi ya watu.
Mashine zinapotumika gharama zinapungua. Kazi ya mashine ni kupunguza gharama na kuokoa muda.

Hayo majengo ya zamani ni kweli yalitumia nguvu kazi, lakini pia yalitumia miaka mingi sana kuyajenga mpaka yakamilike. Na pia kuchoronga hiyo michoro /urembo walihitajika wataalamu hasa sio mafundi kama wa sasa. Kwahiyo gharama ilikua kubwa.

We sema saa nyingine walikua wanatumia watumwa kwahiyo gharama inapungua.

 
Wewe hujatembea ndio maana unasema majengo ya zamani yanapendeza kuliko ya Sasa hivi mpo serious kweli halafu kwanini mnaushamba wa kusifia vitu vya zamani hata kama havina hiyo sifa
Tusiongee sana, wewe uliyetembea tuwekee picha ya nakshi za kisasa...ilimradi usutuletee mable na tiles oriented buildings

Tupo hapa tunasubiri
 

Vipi kuhusu huu mlango? Umeona size ya urefu wake?

 
Hizo ni tofauti kati ya mashine na nguvu kazi, lakini ubora na kudumu kwa muda mrefu ndyo sifa kuu ya majengo ya zamani
 
Sasa kuna ubunifu gani wa kuvutia hapa zaidi ya vioo tu?
Hivyo vioo ndio ubunifu wenyewe wa kuvutia unafikiri Sasa hivi watu wanashindwa kujenga kama hayo majengo ya zamani sema hayawezi kuwa na fashion mzee tunaenda na dunia inapoenda sio kuganda tu milele kama unaona kioo sio ubunifu basi wewe katika wale washamba wa duniani upo namba 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…