Je, ni kweli wanaume masikini wana hasira na majeuri kama asemavyo dada kwenye Video?

Je, ni kweli wanaume masikini wana hasira na majeuri kama asemavyo dada kwenye Video?

Wanaume masikini wana hasira, wana jeuri.
View attachment 3692540
Sio kweli hiii 😅😅😅
Kuna mambo kadhaa hupelekea hasira na sio kwa wanaume pekee hata Wanawake wasio kuwa na wanaume hao ndio wana hasira ile mbaya

Hasira hutokana na
1. Shinikizo la maisha hasa pale unaposhindwa kumudu gharama za maisha kama Kodi, Chakula, Mavazi nk haya mambo hupelekea hasira za haraka mnoo

2. Hisia za kuahindwa kufanya jambo fulani na kulitimiza au likaenda kinyume na ulivyotarajia hupelekea hasira pia na si kwa wanaume pekee hata mwanamke pia

3. Unapojitahidi kudhibiti hali fulani kwenye maisha nayo hupelekea hasira pia hata humu tunaona watu wanalazimisha attentions, wanalaImisha kukubalika lakini inakuwa ndivyo sivyo wanaishia kutoa lugha chafu na kuishia kupewa BAN

4. Aibu ya kuomba msaada wakati mwingine nayo husababisha upweke na kupelekea hasira pia

5. Malezi na makuzi ya utotoni nayo ni changamoto pia unapokutana na mazingira tofauti na ulivyokulia na kulelewa.

Kwahiyo kusema umaskini husababisha au huwa chanzo cha hasira sio kweli, mbona kuna watu wana pesa na kila kitu lakini bado wana hasira na ujeuri mwingi tu. Sababu ni nyingi sana ambazo huwa ni vyanzo vya hasira tena si kwa wanaume hata wanawake.
 
Back
Top Bottom