Tetesi: Je, ni kweli watu wa Afrika Mashariki wanatamani nchi moja ya Afrika Mashariki kutoka EAC?

Tetesi: Je, ni kweli watu wa Afrika Mashariki wanatamani nchi moja ya Afrika Mashariki kutoka EAC?

Nchi za weusi muungano ni jambo muhali.

Jambo la muungano ni la baraka tele, tatizo ubinafsi na roho zetu waAfrika.

Ukiangalia mfano S.Sudan, wao kwa wao wana bifu la madaraka kwa ajili ya matumbo yao, sasa watu kama hao waliojaa ubinafsi wa kufa mtu wanawezaje kushawishika kuachia nyadhifa zao na kisha kumezwa na muungano?
 
Kuwa nchi moja haiwezekani ila mambo mengine kama sarafu moja, umiliki wa miundombinu ya pamoja na free movement of labour na capital itakuja wezekana huko mbeleni!
Tanganyika ilazimishe muungano kamili na nchi za EA kama inavyoibana Zanziibar. Uwezo tunao na nia tunayo. CCM oyee.
 
Wabongo hatutaki hiyo kitu kabisa. Ikiruhusiwa tu, ming'ombe yote ya Kenya, Burundi na Rwanda italetwa huku na kusababisha migogoro ya ardhi.
Kwa ajili ya amani yetu, raia wao wengi watahamia kwetu na kusababisha mzigo mkubwa kwa serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Watavamia misitu na kukata miti hovyo kupata maeneo ya kufugia na mashamba na upo ushahidi mkubwa baadhi yao kujihusisha na ujangili na ujambazi. Na hawa ni waingizaji wakubwa wa silaha haramu nchini. Hivyo watajishahusi na vitendo mbalimbali vya kihalifu ili kupata utajiri wa haraka haraka.
Kwanini unahisi rwanda inamifugo mingi kiasi hicho wakat Tanzania ndo tunaongoza
 
Kama wapemba hawajawahi kuufurahia muungano hizo nchi zote hazitaweza kufirahia muunganiko ila kama ingiwezekana tungekuwa mbali sana kwa kila sekta maana hii mipaka inaturudisha nyuma sana
Muungano wenyewe uwe Kama huu Tanzania? Hapana.
 
Free movement of Labour?sio rahisi hio brother/sister.
Mkuu inawezekana sana sema sie watz tunawahofia tu bure wakenya hebu itazame Tanganyika na Zanzibar kikatiba imekaa kama state Union lkn kiuhalisia kabisa ni integration ambayo ni economic union unaona kabisa free movement of capital na labour, enh bakheresa kawekeza Tanganyika na hata watanganyika wengi wamejenga mahotel zenji, pia watanganyika kibao wameajiriwa kwny mahotel zenji hiyo ni free movement of labour kabisa kwa kutumia sheria hizohizo
 
Tanganyika ilazimishe muungano kamili na nchi za EA kama inavyoibana Zanziibar. Uwezo tunao na nia tunayo. CCM oyee.
Labda wao ndo watulazimishe sio sisi, make wao muungano wanaulilia sana hasa economic Union ila tz ndo tumekuwa kikwazo tunachelewesha mchakato!
 
Kuna viongozi wanataka.kufia humo humo kwenye urais wanakoelekea mpaka wataanza kuanikwa nje na kurudishwa ndani kama mazao ila wao watatumia magodoro kuwaanika nje, wakae huko huko, ona kama south Sudan anazunguka yule yule hata anachokifanya mie hata sielewagi zaidi ya kugombana wao viongozi utazani club za mpira
 
Back
Top Bottom