Baadhi ya watu hudai kwamba wanawake hutumia muda mwingi kufikiria namna ya kujenga maisha, kama vile jinsi ya kuwa na maisha mazuri. Lakini kwa upande mwingine wanaume wanaonekana kutumia muda mwingi kufikiria suala la kimapenzi zaidi. Hivyo mwanamke huonekana ni mtu wa kufikiria mambo mazito wakati mwanaume anafikiria mambo mepesi mepesi tu! Je kuna ukweli katika hilo?